Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali magharibi mwa Sudan
Jimbo la Darfur Magharibi la magharibi mwa Sudan limekuwa likishuhudia mapigano makali, huku mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea kufanyika. Hayo yameripotiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) ambalo limeongeza katika taarifa yake kwamba takriban watu 700 wameripotiwa kuuawa, 100 walijeruhiwa na wengine 300 wamepotea katika Jimbo la Darfur…
Al-Sisi amuhutubia mkuu wa CIA: ‘Cairo katu haitashiriki katika uharibifu wa Hamas’
Rais wa Misri alikataa pendekezo la mkuu wa CIA kuhusu utawala wa usalama wa Ukanda wa Gaza na kutangaza kuwa serikali yake haitahusika kamwe katika uharibifu wa Hamas. Kulingana na mkutano kati ya William Burns, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani linalojulikana kama CIA, na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini Cairo, vyanzo…
Afrika Kusini yatoa onyo kwa balozi wa utawala wa Kizayuni
Serikali ya Afrika Kusini imetoa onyo kwa balozi wa utawala wa Kizayuni kutokana na matamshi na kauli yake isiyoridhisha. Afisa wa sera za kigeni wa Afrika Kusini aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumatano kwamba serikali ya nchi hiyo imemwita balozi wa Israel kwa lengo la kumkemea rasmi kwa kutoa kauli za kuudhi….
Ongezeko la vyama vya siasa Kenya kabla ya uchaguzi wa 2027, mradi wa kibiashara?
Ongezeko la vyama vya siasa vinavyojiandikisha nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 limetajwa kuwa ni mradi wa viongozi wa vyama hivyo kwa ajili ya kujipatia kitita kikubwa cha fedha za walipakodi wa Kenya. Ripoti zinasema, idadi kubwa ya vyama vya kisiasa vinavyosaka usajili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027 ni kiashiria cha jinsi mabilioni…
Umoja wa Afrika wamuunga mkono katibu mkuu wa UN kuhusu Palestina
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ametangaza uungaji mkono wake kamili kwa Kaitbu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutokana na ‘uongozi na msimamo wake imara’ kuhusu hujuma ya kijeshi ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Moussa Faki Mahamat ameandika katika ukurasa wake wa X kwamba: “Naunga mkono kikamilifu uongozi…
Uganda yataja onyo la Marekani dhidi yake kuwa kichekesho
Uganda imekejeli na kukosoa tahadhari iliyotolewa na Marekani iliyodai kuwa ni hatari kufanya biashara na kuwekeza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Godfrey Kabbyanga, Waziri Msaidizi wa Habari wa Uganda amewataka wawekezaji wapuuze inadhari hiyo ya Marekani akisisitiza kuwa, maonyo kama hayo hayaendani na hali halisi katika nchi hiyo ya Afrika. Juzi Jumatatu, Wizara ya…
Mlipuko wa ugonjwa kipindupindu wakumba majimbo matatu ya Sudan
Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umeripotiwa kuyakumba majimbo matatu ya Sudan. Takriban visa 817 vinavyoshukiwa kuwa maradhi ya kipindupindu vimeripotiwa katika majimbo matatu ya Sudan, vikiwemo vifo 35. Visa hivyo viliripotiwa katika majimbo ya Gedaref, Kordofan Kusini na Khartoum, tovuti ya habari inayomilikiwa kibinafsi ya al-Rakoba iliripoti, ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO). Mwanzoni mwa…
Rais Ruto aongoza Wakenya kuadhimisha Siku ya Mashujaa huku wanne wakifa katika mkanyagano
Rais William Ruto wa Jamhuri ya Kenya leo aliwaongoza Wakenya kusherehekea Siku ya Mashujaa yaliyotilia mkazo mpango wa afya bora kwa wote, huku watu wanne wakiripotiwa kuaga dunia kutokana na mkanyagano kwenye maadhimisho hayo. Akihutubia katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mjini Kericho, Rais Ruto Rais alizindua mpango mpya wa huduma ya afya kwa wote uitwao…