Kaburi la umati lenye miili 25 laguduliwa kaskazini mwa Malawi
Malawi imetangaza kuwa, imegundua kaburi la umati kaskazini mwa nchi hiyo lenye mabaki ya watu 25 wanaoshukiwa kuwa wahamiaji kutoka Ethiopia. Taarifa iliyotolewa na polisi ya Malawi imeeleza kuwa, “kaburi hilo liligunduliwa Jumanne jioni, lakini tulilizingira na kuanza kufukua jana. Kufikia sasa, tumegundua miili 25. Hayo yameelezwa na msemaji wa polisi ya Malawi Peter Kalaya…
Uganda yafunga wilaya 2 ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola
Serikali ya Uganda imetangaza habari ya kuziweka wilaya mbili za nchi hiyo katika karantini, kwa lengo la kudhibiti mripuko wa virusi vya Ebola unaoshuhudia katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa. Katika utekelezaji wa karantini hiyo, mabaa, maabadi, na kumbi za starehe zitafungwa kwa wiki tatu katika wilaya…
Wahadhiri wa vyuo vikuu Nigeria wahitimisha mgomo wao wa miezi 8
Muungano wa Kitaaluma wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu vya Serikali Nigeria (ASUU) umetangaza leo Ijumaa kuhitimiha mgomo wao wa miezi 8. ASUU ambayo ni taasisi mwavuli ya wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya serikali kote Nigeria, imetoa taarifa hiyo leo katika mtandao wa kijamii. Hata hivyo bado haijabainika wazi ni lini masomo ya vyuo vikuu yaatanza tena rasmi…
Mahakama Kenya yatoa waranti wa kutiwa mbaroni Wazayuni wawili kwa kubaka watoto wadogo
Mahakama nchini Kenya imetoa waranti wa kutiwa mbaroni Wazayuni wawili kwa makosa ya kubaka watoto wadogo na vitendo vya uasherati huko Shanzu katika Kaunti ya Mombasa. Wazayuni hao wanaojulikana kwa majina ya Koren Avraham na Ashush David walikimbia nchini Kenya kwa madai ya matibabu baada ya kupewa dhamana ya Shilingi laki mbili za Kenya na hadi…
Sheikh Zakzaky: Saudia ilihusika katika mauaji ya wafuasi wa Ahlul Bait (AS) huko Zaria
Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, Saudi Arabia ilikuwa na nafasi katika mauaji ya wafuasi wa Ahlul Bait (as) katika mji wa Zaria mwaka 2015 yaliyotekelezwa na jeshi la Nigeria. Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema katika mahojiano maalumu na televisheni ya Al-Alam, ambayo maelezo yake yatatangazwa baadaye, kwamba mauaji ya Zaria…
Al-Azhar yalaani kuchomwa moto Qurani na walowezi wa Kizayuni
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al Azhar cha nchini Misri kimelaani kile ilichokitaja kuwa ugaidi za Kizayuni, baada ya Walowezi wa Kiyahudi kuchoma moto Qurani Tukufu katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na al-Azhar imeeleza kuwa, kitendo hicho cha kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu…
Kenya na Tanzania zaazimia kuimarisha uhusiano katika safari ya Ruto
Baada ya mazungumzo hayo, wawili hao wamehutubua waandishi wa habari katika Ikulu mjini Dar es Salaam na kubainisha nukta kadhaa muhimu. Marais hao wametoa maagizo kwa mawaziri wa uwekezaji kuhakikisha wanaondoa vikwazo 14 vya biashara baina ya nchi hizo. Rais wa Kenya amesema yale mabishano yaliyokuwepo baina ya Tanzania na Kenya wameyaweka nyuma. Rais Ruto…
Ruto, Raila Kumenyania Kiongozi Wa Wengi Bungeni
MVUTANO mkali unatazamiwa hii leo Jumanne Bungeni kati ya kambi ya Rais William Ruto ya Kenya Kwanza na Azimio ya Raila Odinga kuhusu kiongozi wa wengi huku pande zote mbili zikidai wadhifa huo. Wadhifa huo unaong’ang’aniwa na mirengo hiyo miwili mikuu nchini tayari umevutia Spika wa Bunge Moses Wetang’ula wa Kenya Kwanza anayetazamiwa kuamua ni…