Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran awasali nchini Mali na kuonana na wenyeji wake
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anaendelea na ziara yake ya kuzitembelea nchi za Afrika na tayari ameanza mazungumzo na viongozi wa Mali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Hossein Amir-Abdollahian ameandamana na ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi wa…
Jinai mpya ya Marekani Somalia, Biden ameua Wasomali 465
Shirika linalochunguza mashambulizi ya anga ya kimataifa limefichua kuwa Marekani inaficha idadi halisi ya vifo vya raia nchini Somalia na kwamba idadi ya waliopoteza maisha katika nchi hiyo ya Afrika ni mara 30 zaidi ya ile iliyotangazwa na Pentagon. Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya “Truthout”, mashambulizi ya anga ya Marekani nchini Somalia katika…
Odinga aenda mahakamani kupinga matokeo ya urais Kenya
Mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya chama cha Muungano wa Azimio la Umoja wa One Kenya, Raila Odinga amewasilisha mahakamani shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC hivi karibuni. Odinga ameongozana na mgombea mwenza, Martha Karua, na vigogo wengine wa muungano huo akiwemo Kalonzo…
Tumepata Ushahidi Wa Kubatilisha Ushindi Wa Ruto – Mawakili
MAWAKILI wa mgombea urais wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga wamesema kuwa, wamekusanya ushahidi wa kutosha kuwawezesha kubatilisha ushindi wa Rais Mteule William Ruto katika Mahakama ya Juu. Mmoja wa mawakili hao, Ndegwa Njiru jana Ijumaa alifichua wako tayari kuthibitisha kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa urais. “Tumepata ushahidi wa kutosha…
Makumi ya magaidi wakufurishaji waangamizwa nchini Burkina Faso
Jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa, limeangamiza magaidi 100 wakufurishaji katika operesheni za kijeshi lilizofanya kwa nyakati tofauti katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Shirika la habari la Tasnim limenukuu taarifa ya jeshi la Burkina Faso ikitoa ufafanuzi kwa kusema, operesheni zilizoangamiza magaidi hao 100 wakufurishaji zimefanyika kwenye maeneo mbalimbali na kwa nyakati tofauti…
Viongozi wa Jumuiya ya SADC wahamasisha ukuaji uchumi na kilimo
Mkutano wa 42 wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ulimazilika jana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Kinshasa, huku wakuu wa jumuiya hiyo wakihamasisha ukuaji wa uchumi, kilimo na juhudi zaidi katika sekta ya madini. Mkutano wa mwaka huu ulikuwa na kaulimbiu isemayo “kuhamasisha viwanda…
Mali yasema Ufaransa inasaidia magaidi, yaitisha kikao Baraza la Usalama
Mali imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano wa dharura ili kusitisha kile inachokitaja kuwa ni “vitendo vya uchokozi” vinavyofanywa na Ufaransa kwa kukiuka mamlaka yake, kuunga mkono makundi ya magaidi wakufurishaji na ujasusi. Barua iliwasilishwa kwa waandishi wa habari na Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali siku ya Jumatano baada…
Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa waondoka Mali
Mabaki ya wanajeshi wa Ufaransa waliondoka nchini Mali jana Jumatatu, kuashiria mwisho wa Operesheni ya Barkhane katika nchi hiyo ya eneo la Sahel barani Afrika. Taarifa ya Vikosi vya Jeshi la Ufaransa imesema, askari wa mwisho wa kikosi cha Barkhane waliokuwa katika ardhi ya Mali wameondoka na kuvuka mpaka baina ya nchi hiyo na Niger….