Kampuni 500 kushiriki maonyesho Mara
Musoma. Zaidi ya kampuni 500 kutoka ndani na nje ya nchi zinatarajiwa kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya ‘Mara International Business Expo’ yatakayofanyika mkoani Mara mwezi Septemba mwaka huu. Maonyesho hayo yanayoandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara yanatarajiwa…
Watanzania waitwa kutafiti mgogoro wa Israel, Palestina
Haya ni maneno ya Balozi wa Palestina nchini Tanzania alipowaita Watanzania kutafiti mgogoro wa Israel, Palestina. Dar es Salaam. Ubalozi wa Palestina nchini umewakaribisha Watanzania kufanya tafiti zaidi kuhusu mgogoro wa Mashariki ya Kati ili kujua ukweli wa historia kati ya Israel na Palestina. Wito huo umetolewa na balozi wa Palestina nchini, Hamdi Mansour AbuAli…
WHO, CDC kuchunguza ugonjwa usiojulikana Lindi
Dar es Salaam. Wakati timu ya wataalamu kutoka nje ikitarajiwa kuanza uchunguzi kubaini ugonjwa usiojulikana Lindi, Wizara ya Afya imesema sampuli za vipimo vya maabara zilizochukuliwa kutoka kwa wagonjwa zimeonyesha siyo ugonjwa wa Ebola, Maburg wala Uviko-19. Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Julai 15, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kwenye Kikao cha 22…
Balozi Palestina aipongeza CCM
Haya ni Mazungumzo ya Balozi wa Palestina nchini TAnzania akipongeza uhusiano wa Tanzania na Palestina BALOZI wa Mamlaka ya Palestina nchini, Hamdi Mansour AbuAli pamoja na mwanaharakati wa haki za binadamu Mashariki ya Kati, Dk. Uri Davis wamekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa msimamo wake wa kuunga mkono jitihada za Wapalestina katika kupigania haki zao….
Sonko aruhusiwa Kuwania Ugavana wa Mombasa, Presha kwa Abdulswamad Shariff Nassir
FARAAN:Majaji watatu wa Mahakama Kuu mnamo siku ya Jumatano tarehe 13 July 2022 walimruhusu aliyekuwa Gavana wa Nairobi, Mike Sonko kuwania wadhifa huo Mombasa, hatua inayotarajiwa kumtia presha mwaniaji wa ODM Abdulswamad Shariff Nassir. Bw. Nassir amekuwa kifua mbele kwenye azma ya kumrithi Gavana Ali Hassan Joho, lakini hatua ya majaji Olga Sewe, Stephen Githinji…
Makubaliano ya utawala wa Kizayuni ya kuikabidhi Saudi Arabia visiwa vya Misri
Utawala wa Kizayuni umeafiki mpango wa jumla wa kuikabidhi nchi ya Saudi Arabia visiwa viwili vya Misri. Shirika la Habari la Kimataifa la Fars limetoa ripoti kua; tovuti ya Marekani imeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni umeafiki mpango wa jumla kuhusu hadhi ya kisheria ya visiwa viwili vya Misri katika Mlango wa Bahari wa Tiran. Hatua…
Vyombo vya habari vya Kizayuni: Somalia inajaribu kuafikiana na Tel Aviv
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vilidai kwamba serikali ya Somalia inajaribu Kurekebisha mahusiano na utawala huo na kujaribu kuurudisha katika hali ya kawaida. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Fars, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vilidai kuwa Mogadishu imeamua kuchunguza suala la kuhalalisha uhusiano na utawala…
Balozi wa Palestina aitaka jumuiya ya kimataifa kuilaani Israel
Haya ni maneno ya Balozi wa Palestina nchini Tanzania akiitaka Jumuiya ya kimataifa ilaani vitendo vya utawala haramu wa Israel kama inavyolaani vitendo vya Russia huko Ukraine, Dar es Salaam. Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali ameitaka jumuiya ya kimataifa kulaani vitendo vya Israel kukiuka makubaliano na Palestina kama ambavyo wamekuwa wakilaani uvamizi wa…