Mahakama yaahirisha kesi ya Chadema, Polisi
Dodoma. Kesi ya maombi madogo ya jinai inayowakabili Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Kamanda wa Polisi (RPC) na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) Dodoma imeahirishwa baada ya washtakiwa hao kutofika mahakamani. Katika shauri hilo la maombi madogo ya jinai namba 25/2022, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeiomba Mahakama…
Zambia kujenga bomba la dizeli kutoka Tanzania
Zambia imeanza kujenga bomba lenye urefu wa kilomita 700 (maili 435) ili kuingiza mafuta ya dizeli kutoka nchi jirani ya Tanzania ambapo uwekezaji wa awali wa mradi huo ni dola milioni 300. Waziri wa Nishati wa Zambia Peter Kapala alisema Jumapili kwamba bomba hilo jipya litaenda sambamba na la sasa lakini litakuwa la kisasa zaidi….
Vodacom yamtangaza bosi mpya Mtanzania
Dar es Salaam. Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imemtangaza Hilda Bujiku kuwa kaimu mkurugenzi mtendaji akichukua nafasi ya Sitholizwe Mdlalose aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa miezi 10. Mdlalose aling’atuka kwenye nafasi hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom nchini Afrika Kusini. Hilda anapokea kijiti akiwa ni Mtanzania na mwanamke wa kwanza kushika nafasi…
Gesi inavyobana matumizi na kufungua fursa
Mtwara. Matumizi ya gesi asilia kwenye malori 256 ya kiwanda cha saruji cha Dangote yamesaidia kuokoa takriban Sh5 bilioni iwapo magari hayo yangetumia mafuta kati ya Machi 2021 hadi Juni. Uchambuzi uliozingatia mwenendo wa bei za mafuta katika siku za hivi karibuni, kiwanda hicho kingetumia zaidi ya Sh11 bilioni lakini gesi imeokoa asilimia 45 ya kiasi…
Qnet yawaponza walimu, wafukuzwa kazi
Geita. Tume ya utumishi wa walimu wilayani Geita mkoani Geita imewafukuza kazi walimu wanane kwa utoro kazini. Walimu hao ambao sita ni wa shule za msingi na wawili wa sekondari, wanadaiwa kujishughulisha na biashara za Qnet badala ya kumtumikia mwajiri huku wengine wakidaiwa kuathiriwa na biashara hizo baada ya kujikuta wanadaiwa na wafanyakazi wenzao waliowaingiza kwenye…
Tanzania yauza tani 10,000 za nyama Bara la Asia
Arusha. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema katika kipindi cha miezi sita Tanzania imeuza nyama tani 10,000 katika nchi za Bara la Asia tofauti na miaka ya nyuma. Waziri Ndaki ameyasema hayo leo Julai 4 wakati ya akifungua warsha ya siku saba ya wataalamu wa sekta ya mifugo kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo…
Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu TPA
Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kuwa haridhidhwi na kasi ya utendaji wa bandari nchini, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi. Taarifa iliyoptolewa jana Jumatatu Julai 4, 2022 na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa nafasi Hamissi inachukuliwa…
Nassir alenga Kufufua Uchumi wa Mombasa
FARAAN:Mbunge wa Mvita Bw Abdulswamad Nassir ambaye anagombea ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya ODM, amewahakikishia wawekezaji wa utalii kuwa atafufua sekta hiyo kwa kupunguza ada za mahoteli na leseni. Alisema uchumi wa Mombasa lazima ufufuliwe kupitia sekta ya utalii. “Tutahakikisha washikadau wanafanya biashara bila ya kuhangaishwa, serikali yangu itashirikiana na mwekezaji ambaye ataweza…