AFRIKA

Rais Mwinyi ayakaribisha Madhehebu ya Bohora kuwekeza Zanzibar

Rais Mwinyi ayakaribisha Madhehebu ya Bohora kuwekeza Zanzibar

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya mazungumzo na kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora (Dawoodi Bohoras) duniani, Syedna Muffaddil Saifuddin na kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa dhehebu hilo kuja kuekeza Zanzibar. Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumapili Julai 3, 2022 Ikulu ya Zanzibar ambapo kiongozi huyo wa Madhehebu hayo akiwa ameambatana ujumbe wake…

Mambo sita ya bajeti yaliyogusa Watanzania

Mambo sita ya bajeti yaliyogusa Watanzania

Dodoma. Unaweza kuita bajeti ya 2022/2023 ni bajeti ya wananchi kutokana na mambo sita makubwa yaliyozingatiwa, ikiwamo fedha nyingi kuelezwa kuwa itapelekwa kwenye wa miradi inayogusa watu wengi na kulenga kupunguza makali ya maisha kwa Watanzania. Mambo mengine yaliyozingatiwa katika bajeti hiyo, ni kuongeza bajeti katika sekta zinazohusu watu wengi na Serikali kukubali kusikiliza maoni ya…

Bilioni 25 za Uviko-19 zapelekwa kukamalisha ujenzi Veta

Bilioni 25 za Uviko-19 zapelekwa kukamalisha ujenzi Veta

Dodoma. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema kati ya Sh64.9 bilioni ilizopewa wizara hiyo kutoka fedha za Uviko-19, Sh20 bilioni zilitengwa kwa ajili ya umaliziaji wa vyuo 25 vya ufundi vinavyojengwa katika wilaya mbalimbali nchini. Kipanga ameyasema hayo leo Jumapili Julai 3, 2022 wakati Kamati ya Bunge ya Bajeti ilipotembelea ujenzi…

Sita wafa ajali ya gari Dodoma

Sita wafa ajali ya gari Dodoma

Dodoma. Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha gari ndogo kugonga na mkokoteni uliokuwa unavutwa na ng’ombe katika Kijiji cha Lugala Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma leo Jumapili Julai 3, 2022. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo huku akiahidi kutoa taarifa kamili baadaye. Kamanda amesema yuko…

Watu sita wa familia moja wauawa Kigoma

Watu sita wa familia moja wauawa Kigoma

Kigoma. Watu sita wa familia moja wameuawa kwa kukatwa sehemu mbalimbali za miili yao kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma mkoani Kigoma. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Julai 3, 2022. Sindano amesema katika mauaji hayo…

Nchi za Afrika Magharibi zajadili vikwazo vya baada ya mapinduzi ya kijeshi

Nchi za Afrika Magharibi zajadili vikwazo vya baada ya mapinduzi ya kijeshi

Viongozi wa Afrika Magharibi wanakutana leo Jumapili kutathmini mustakabali wa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi tatu ambako jeshi limechukua mamlaka. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeweka vikwazo vikali vya kiuchumi na kifedha dhidi ya Mali na adhabu ndogo kwa Burkina Faso na Guinea baada ya wanajeshi kuchukua madaraka katika nchi hizo….

Shaka aipongeza MNH kufanikisha upasuaji pacha walioungana

Shaka aipongeza MNH kufanikisha upasuaji pacha walioungana

Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kufanikisha upasuaji wa kutenganisha watoto Neema na Rehema walioungana na kuwaweka katika uangalizi mzuri. Upasuaji huo uliodumu kwa kwa saa saba, ulifanikiwa licha ya changamoto kubwa kwa watoto hao kuungana ini, moyo na baadhi ya tishu za ndani…

Miaka 30 ya vyama vingi na dai la katiba

Miaka 30 ya vyama vingi na dai la katiba

Wakati nchi ikitimiza miaka 30 tangu irejeshe rasmi mfumo wa siasa za vyama vingi, mjadala mwingine wa katiba mpya umeibuka, ingawa baadhi ya wadau wanasema kumekuwa na maendeleo ya demokrasia chini ya mfumo wa sasa. Kilio hicho cha katiba mpya kilikuwepo mwaka 1992 wakati nchi ikielekea kufanya maamuzi ya kuondokana na mfumo wa chama kimoja…