AFRIKA

Mkunga asimamishwa kazi kwa kutelekeza wajawazito

Mkunga asimamishwa kazi kwa kutelekeza wajawazito

Dar es Salaam. Mkunga wa zahanati ya Kashai iliyopo Manispaa ya Bukoba, Leticia Muganyizi amesimamishwa kazi kwa kipindi cha miezi mitatu na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kwa kosa la kutelekeza akina mama wajawazito. Tukio hilo lililotokea jana Julai Mosi, 2022 limesababisha adha kwa wajawazito hao na hivyo kukiuka sheria ya uuguzi na ukunga…

Tani 60,000 za makaa ya mawe kusafirishwa nje ya nchi

Tani 60,000 za makaa ya mawe kusafirishwa nje ya nchi

Songwe. Waziri wa Madini, Dk Dotto Biteko amesema Serikali inatarajia kusafirisha tani 60,000 za makaa ya mawe kupelekwa nje ya nchi baada wa Shirika la Madini Taifa (Stamico) kuanza uzalishaji katika mgodi wa Kiwira-Kabulo Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe. Dk Biteko amesema hayo leo Jumamosi Julai 2, 2022 alipofanya ziara kukagua miundombinu katika mgodi…

Watano wafa ajalini, 17 wajeruhiwa Tabora

Watano wafa ajalini, 17 wajeruhiwa Tabora

Tabora. Watu watano wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana Ijumaa jioni Julai Mosi, 2022 katika kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora. Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema basi hilo la Sasebosa lilikuwa linatoka mkoani Mbeya kwenda Tabora. Kamanda Abwao amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika…

Mabadilishano ya kibiashara baina ya Iran na Tanzania yameongezeka kwa 120%

Mabadilishano ya kibiashara baina ya Iran na Tanzania yameongezeka kwa 120%

Balozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesema, mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili katika mwaka uliopita yaliongezeka kwa asilimia 120. Hossein Alvandi ameyasema hayo katika kikao cha wawakilishi wa vyama vya wafanyabiashara wa Iran na Tanzania kilichofanyika kwa njia ya intaneti na akaongezea kwa kusema, kuna fursa na mazingira…

Pacha walioungana watenganishwa Muhimbili

Pacha walioungana watenganishwa Muhimbili

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikisha upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha walioungana kifuani Rehema na Neema. Upasuaji huo uliodumu kwa saa 7, ulioanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 9 alasiri, umefanikiwa licha ya ugumu na changamoto kubwa kwa watoto hao kuungana ini, moyo na baadhi ya tishu za ndani. Upasuaji huo…

Jeshi la Nigeria laua wabeba silaha 82 jimboni Zamfara

Jeshi la Nigeria laua wabeba silaha 82 jimboni Zamfara

Jeshi la Nigeria limetangaza habari ya kuangamiza makumi ya wanachama wa genge moja la wabeba silaha katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Wizara ya Ulinzi ya Nigeria imesema jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuua wanachama 82 wa genge hilo katika operesheni ya mashambulizi ya anga iliyopewa jina la “Hadin Kai”. Taarifa ya…

Hospitali ya Mkapa kuzalisha mitungi 400 ya gesi kwa siku

Hospitali ya Mkapa kuzalisha mitungi 400 ya gesi kwa siku

Dodoma. Hospitali ya Benjamin Mkapa imezindua mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya Oxygen utakaozalisha mitungi ya gesi 400 kwa siku. Mtambo huo umezinduliwa leo Ijumaa Julai Mosi, 2022 na jijini Dodoma na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu huku akimwagia sifa hospitali hiyo kwa utoaji huduma bora na kuahidi kuipandisha hadhi kuwa ya Taifa. “Popote nitakapokwenda nitasema…

Ukataji wa tiketi mtandao wasuasua, wapiga debe wahofia vibarua

Ukataji wa tiketi mtandao wasuasua, wapiga debe wahofia vibarua

Moshi. Ikiwa leo ndio siku rasmi ambapo wadau wa usafiri wa masafa marefu walitakiwa kuanza rasmi mfumo wa ukataji wa tiketi kwa njia ya mtandao bado muitikio umekua wa kusuasua huku wapiga debe wakiendelea na kazi za ukataji tiketi za kawaida. Mwananchi ilifika katika kituo kikuu cha Mabasi Moshi Mjini na kushuhudia wapiga debe wakiendelea na…