Rais Mwinyi aeleza Tanzania ilivyoboresha mazingira ya biashara
Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Tanzania imechukua hatua kadhaa kuboresha mazingira ya biashara nchini humo. Rais Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara, wawekezaji wa kitanzania na wadau wa Bandari za Tanzania jijini Bunjubura nchini Burubdi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea leo Ijumaa Julai Mosi, 2022 na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais…
Waziri Nape awataka wananchi Msomera wasiuze ardhi
Handeni. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka wananchi waliohamia kijiji cha Msomera kutoka Ngorongoro wasiuze ardhi waliopewa na Serikali. Waziri Nape amesema hayo leo Ijumaa Julai Mosi 2022 alipofanya ziara yake ya siku moja katika kijiji cha Msomera kwaajili ya kukagua miundombinu iliyojengwa na kuzungumza na wananchi hao. Amesema kuhusu…
Rais Samia amwapisha Mkuu wa Majeshi mpya, Mabeyo kupangiwa majukumu mengine.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemwapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda huku akiahidi kumpangia majukumu mengine CDF aliyemaliza muda wake, Jenerali Venance Mabeyo. Hafla ya la kumwapisha Jenerali Mkunda ilifanyika leo Alhamisi Juni 30, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam. Mkuu huyo wa nchi pia amemwapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi…
Wanunuzi wa pamba kutaifishwa mizani kwa watakaofanya udanganyifu
Bariadi. Katibu wa chama cha wanunuzi wa zao la pamba nchini, Boaz Ogola amebariki maamuzi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ya kuitaifisha mizani itakayofanya udanganyifu katika ununuzi wa pamba msimu huu. Ogola ameyasema hayo leo Juni 30, 2022 katika mahojiano na waandishi wa habari ambapo ameelezea hatua hiyo kuwa inalenga kuboresha maslahi ya…
Pacha walioungana kifuani kufanyiwa upasuaji leo.
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo inatarajia kuwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha pacha walioungana kifuani. Upasuaji huo unakadiriwa kutumia saa saba na utafanywa na wataalamu wa afya 31 kutoka Tanzania na Ireland ambao wanatokea Shirika la Operation Child Life. Tanzania itakuwa nchi ya tatu baada ya Misri na Afrika Kusini katika bara la Afrika…
Kafulila aagiza waliotafuna fedha za makusanyo ya Halmashauri wasakwe
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ameagiza kusakwa na kuwekwa ndani watu wote ambao wanadaiwa kuhusika katika upotevu wa kiasi cha Sh milioni 38 za makusanyo ya ushuru kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Kafulila ametaka kila mtu ambaye amehusika kwenye upotevu wa fedha hizo, akamatwe kisha awekwe ndani na atatoka mara baada ya…
Mabaharia nchini wajivunia walivyojitoa kwa taifa wakati wa Uviko-19
Mabaharia nchini wamejivunia jinsi walivyotoa rehani maisha yao katika kipindi cha Uviko-19 ili kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kupandisha kiwango cha uchumi wa Tanzania na Dunia kwa ujumla. Mabaharia hao wameeleza hisia zao Juni 29, 2022 ikiwa ni siku chache tangu yalipofanyika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mabaharia yakiwa…
Vigogo wanne wa bandari waburuzwa mahakamani
Dar es Salaam. Waliokuwa wafanyakazi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 1.85 milioni sawa na Sh4.2 bilioni. Washtakiwa hao ni aliyekuwa Ofisa Rasilimali watu, Peter Gawile (58), aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Manununuzi,…