Rais Samia amteua Jenerali Mabeyo
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa uteuzi huo umeanzia leo Alhamisi Juni 30, 2022. Uteuzi huo umekuja muda…
Mjumbe wa UN Kongo alitahadharisha Baraza la Usalama kuhusu hali ya usalama Kongo
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bintou Keita amelitahadharisha Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu machafuko ambayo yanaweza kuibuka mashariki mwa nchi hiyo ambako makundi ya wanamgambo wenye silaha yanaongezeka kila siku. Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la UN, Bintou Keita amesema kuwa, iwapo kundi la waasi wa…
William Ruto na Raila Odinga watofautiana kuhusu mfumo wa IEBC
WAGOMBEAJI wakuu wa urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, William Ruto na Raila Odinga jana walitofautiana hadharani kuhusu mfumo wa kuwatambua wapiga kura siku ya uchaguzi mkuu. Katika mkutano wa wagombea urais na wakuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika mkahawa wa Windsor jana, Dkt Ruto alikubaliana na pendekezo la tume…
Viongozi wa Kenya Kwanza wadai Bandari Zote Nchini Zimeuziwa Dubai
FARAAN: Muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Naibu wa Rais William Ruto sasa unadai Serikali inapanga kukabidhi bandari tatu za Kenya kwa kampuni ya Uarabuni. Kwenye taarifa iliyosomwa na Kinara wa Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi, viongozi wa Kenya Kwanza walisema usimamizi wa bandari za Mombasa, Lamu na Kisumu umepeanwa kwa kampuni kutoka Milki…
Wananchi ‘wamchomoa’ mtuhumiwa mikononi mwa Polisi, wamuua
Morogoro. Mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Ally Ally aliyekuwa akituhumiwa kumuua mwenzake aliyefahamika kwa jina la Kibwana Musa (32) mkazi wa Kijiji cha Kiziwa A, kata ya Kiroka kwa madai ya kumfumania na mwanamke wake, naye ameuawa kwa kupigwa na mawe na kukatwa katwa na mapanga na wananchi wenye hasira kali muda mfupi baada ya kumkamata….
Maombi kina Mdee ridhaa ya kupinga kuvuliwa uanachama kusikilizwa leo
Dar es Salaam. Maombi ya ridhaa ya kufungua shauri kupinga kuvuliwa uanachama ya wabunge 19 wa viti maalum akiwamo Halima Mdee na wenzake yatasikilizwa leoJuni 30, 2022. Mahakama Kuu imepanga kusikiliza maombi hayo leo baada ya Chadema kuondoa pingamizi lake dhidi ya maombi yao ya zuio la muda (kulinda ubunge wao) hadi maombi yao ya…
Umoja wa Afrika watuma waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya
Umoja wa Afrika (AU) umetuma waangalizi kufuatilia uchaguzi mkuu wa Agosti 9 nchini Kenya ambao umepelekea joto la kisiasa kupanda nchini humo. Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema, “Kufuatia mwaliko wa Serikali ya Jamhuri ya Kenya kwa Umoja wa Afrika kuangalia uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Agosti 9, 2022, Tume ya Umoja wa Afrika inatuma…
Katibu Mkuu wa CWT na mwenzake wahukumiwa miezi sita jela
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu nchini Tanzania (CWT), Deus Seif na Mwekahazina wa chama hicho, Abubakari Allawi, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuchepusha Sh 13.9milioni mali ya CWT. Hukumu hiyo imesomwa jana usiku Juni 28, 2022 katika Mahakama ya Hakimu…