EACO yajidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dk Jabiri Bakari (wa pili kutoka kushoto) akiwasilisha hoja kwenye kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) kilichofanyika Bububu, Zanzibar; wengine pichani ni Mtendaji Mkuu wa EACO Dkt. Ally Simba (wa kwanza-kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano-Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo (wa kwanza kulia), na…
Waziri Aweso akemea ubambikaji ankara za maji
Arusha. Wenyeviti wa Bodi za Maji nchini wametakiwa kudhibiti na kuhakikisha wanasimamia mamlaka za maji ili wananchi wasibambikiwe ankara za maji ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na baadhi ya wananchi. Agizo hilo limetolewa leo Juni 29, 2022 na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akifungua mafunzo ya siku tatu ya Bodi na Menejimenti za Mamlaka za Majisafi na Usafi…
Rais ateua Mkuu mpya wa Majeshi
Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na Kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF). Uteuzi huo umefanyika leo Jumatano Juni 29, 2022 ambapo uapisho wa CDF Kakunda unatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Juni 30 saa saba Ikulu jijini Dar es…
Jeshi la Sudan lashambulia eneo linalozozaniwa katika mpaka na Ethiopia
Majeshi ya Sudan yalifyatua mizinga mikubwa wakati wa mapigano katika eneo la mashariki linalozozaniwa la al-Fashaqa linalopakana na Ethiopia. Hayo yamedokezwa na afisa wa Ethiopia huku kukiwa na wasiwasi wa kuibuka tena mvutano baina ya nchi hizo mbili kuhusu mzozo wa muda mrefu katika eneo hilo la mpaka wa pamoja. Jumanne Sudan iliweza kuteka eneo…
Warioba: Katiba irudi kwa wananchi
ar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesisitiza msimamo wake kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba akitaka maoni ya wananchi yapewe kipaumbele. Warioba alisema hayo jana baada ya kutoa maoni yake katika Kikosi Kazi cha maoni ya demokrasia na vyama vya siasa, akitahadharisha maoni ya wananchi yasibezwe. Pia alieleza akishangazwa kuona maoni ya viongozi…
Chadema, kina Mdee kortini tena leo
Dar es Salaam. Waliokuwa wanachama 19 wa Chadema, akiwamo Halima Mdee wanaingia katika mchuano na chama hicho wakati wa usikilizwaji wa pingamizi dhidi ya maombi ya amri ya kudumisha hali ilivyo (kulinda ubunge wao). Mdee na wenzake 18 wamefungua maombi Mahakama Kuu, Masjala Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema (iliyosajiliwa), Tume ya Taifa ya…
Shehena za dawa zakamatwa Dar, zipo za kuongeza nguvu za kiume
Dar es Salaam. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekamata vifaa tiba na dawa zenye thamani ya Sh294,486,590 milioni ambazo hazijasajiliwa zilizohifadhiwa kwenye ghala bubu lililopo eneo la Mtaa wa Kitumbini katika Kata ya Mchafukoge katikakati ya Jiji la Dar es Salaam. Miongoni mwa dawa zilizokamatwa katika shehena hiyo ni pamoja na zile za kuongeza…
Waziri Nape aagiza wananchi kutoa taarifa wanaohujumu minara
Morogoro. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewataka wananchi katika maeneo ilipojengwa minara ya mawasiliano ya simu kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuilinda, kuitunza na kuitumia kwa kuwa uwekezaji huo mkubwa umeigharimu Serikali fedha nyingi. Waziri Nape alisema hayo mjini Morogoro wakati akizindua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Mfuko…