Viongozi wa dini: Toeni ushirikiano mhesabiwe, Sensa siyo ushetani
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike akizungumza na wajumbe wa kamati ya amani ya viongozi wa dini mkoa wa Mwanza wakati akifungua kikao cha mafunzo ya umuhimu wa sensa Mwanza. Baadhi ya viongozi wa dini mkoani Mwanza wamewataka waumini wa dini mbalimbali nchini kujitokeza katika Sensa ya Watu inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 huku wakisema…
Wanaojifanya mawakala wa freemason wakamatwa
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 23 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya utapeli kwa njia ya mtandao. Kukamatwa kwa watu hao ni matokeo ya oparesheni maalum iliyofanywa na kanda hiyo kwa kushirikiana na timu maalumu ya Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni. Operesheni hiyo iliyofanyika…
Mvutano mkali Kwenye mpaka wa Sudan na Ethiopia; Al-Burhan aitishia Ethiopia
Mkuu wa Baraza la Mpito la Sudan amesisitiza kuwa, jibu la nchi yake kwa Ethiopia kuhusu mauaji ya wanajeshi wa Sudan katika eneo la mpaka wa al-Fashqa litadhihiri kwenye medani ya vita. Kwa mujibu wa baadhi ya wanajeshi wa Sudan, mapigano makali yalizuka kati ya wanajeshi wa Sudan na Ethiopia kwenye mpakani mwa nchi hizo…
MwananchiHabari ZaidiKitaifa Zanzibar, Taasisi ya UAE wasaini mikataba kujenga miradi
Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Mfuko wa Misaada wa Sheikh Zayed bin Sultan al Nahyan kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wametiliana saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kisiwani humo. Utiaji wa saini mikataba hiyo ya miradi mitatu katika nyanja za elimu, afya na ustawi wa jamii, umefanyika leo Jumatatu Juni…
Mmoja afa ajalini gari ikiteketea kwa moto
Mbeya. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kunusurika katika ajali baada ya roli lililobeba shehena za mizigo likielekea mkoani Dar es Salaam kuferi breki na kugonga magari manne na kisha kuwaka moto katika mtelemko wa barabara kuu ya Mbeya-Iringa eneo la Pipe line Wilaya ya Mbeya Vijijini. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Urlich Matei amesema…
Kibano kipya kwa wafanyabiashara
Dodoma/Dar. Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2022 unaoanza kujadiliwa leo umependekeza faini ya Sh100,000 kwa kampuni itakayoshindwa kuwasilisha taarifa za wamiliki wanufaika au kuwasilisha ritani. Adhabu hiyo itakayowahusu pia maofisa wa kampuni husika watakaochangia ucheweleshaji huo, itaenda sambamba na Sh10,000 itakayotozwa kila siku itakayozidi kabla ya kulipwa kwa faini husika. Muswada huo utakaojadiliwa bungeni,…
Chadema yaweka pingamizi maombi mapya ya kina Mdee
Dar es Salaam. Chadema imewawekea pingamizi akina Halima Mdee na wenzake katika maombi yao, ya amri ya muda ya mahakama kuizuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Spika wa Bunge kuwavua ubunge baada ya chama hicho kuwavua uanachama. Pingamizi hilo la Chadema litasikilizwa Jumatano Juni 29, 2022 mchana. Hata hivyo, Mahakama hiyo imetoa amri…
Asilimia 70 wanaougua saratani ni wanawake
Dar es Salaam. Wakati wagonjwa wa saratani wakiongezeka nchini, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imesema kati ya wagonjwa wapya 8,000 na wale wa marudio 68,000 waliopokelewa mwaka 2021 asilimia 70 ni wanawake. Licha ya saratani ya kizazi na ile ya matiti zinazowahusu wanawake kuongoza, imeelezwa kuwa wanawake pia wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa katika…