Mtatiro aagiza mwalimu aliyezaa pacha wanne kuhamishiwa mjini
Tunduru. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuanza mchakato wa kumhamishia kwenye shule iliyoko mjini humo Mwalimu Judith Sichalwe mwenye miaka 29 ambaye amejifungua watoto wanne bila upasuaji katika hospitali ya Wamisionari ya Mbesa. DC Mtatiro ametoa maelekezo hayo jana Juni 26 alipomtembelea Mwalimu huyo katika kijiji…
Sheria yaja kudhibiti salio lililotelekezwa kwenye simu, benki
Dodoma. Ili kuzitumia fedha za wateja wasiozitumi akaunti zao za benki au simu za mkononi kwa muda mrefu kutokana na sababu tofauti, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali itakamilisha kuandaa mapendekezo ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali Fedha Zilizotelekezwa mwaka ujao wa fedha. Kwa utaratibu uliopo, mteja ambaye hajaitumia akaunti yake ya…
Rais Samia aeleza Anna Mkapa alivyomuingiza katika siasa
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amebainisha kwamba Anna Mkapa, mke wa Rais mstaafu, Hayati Benjamin Mkapa, ndiye aliyemfanya aingie kwenye siasa. Rais Samia amebainisha hayo leo Jumatatu Juni 27 jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF) ulioanzishwa Juni 1997….
Serikali yapunguza tozo ya ving’amuzi
Dodoma. Serikali imepunguza tozo ya ving’amuzi nchini kufikia Sh500 hadi Sh2000 kwa kadri ya matumizi ya mteja baada ya majadiliano na Kamati ya Bunge ya Bajeti. Kabla ya majadiliano hayo tozo iliyopendekezwa katika makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya serikali 2022/23 ilikuwa Sh1,000 hadi Sh3,000. Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 2022/2023 na Mwenyekiti wa…
Kina Mdee ngoma nzito, wafungua kesi nyingine
Dar es Salaam. Wabunge waliofukuzwa Chadema wameendeleza mapambano ya kisheria mahakamani kupigania uanachama na ubunge wao, baada ya kufungua tena shauri wakiomba ridhaa ya mahakama kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama. Awali, Halima Mdee na wenzake 18 walifungua maombi kama hayo Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria…
Nape mgeni rasmi kongamano maendeleo ya tasnia ya habari
Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kujadili maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Kongamano hilo limeandaliwa na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, likishirikiana na wadau mbalimbali litakafanyika Jumatano Juni…
Mbinu mpya kwa wavuvi nchini Tanzania jinsi ya kukabiliana na majanga
Mwanza. Serikali imewataka wavuvi nchini kuchangamkia fursa kwa kukata bima ili kuwasaidia pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali kwenye shughuli zao. Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki wakati akizindua bima maalumu kwa wavuvi uliofanyika jijini Mwanza. Bima hiyo mpya imezinduliwa kwa ushirikiano wa benki ya NMB na kampuni ya bima ya Britam inahusisha…
Sh 2.2 bilioni kumaliza tatizo la maji Buza
Dar es Salaam. Kukamilika kwa mradi wa maji wa Jet Buza kunamaliza kilio cha muda mrefu cha wakazi wa kata hiyo na maeneo jirani wakitarajia kuachana na utegemezi wa maji ya visima. Mhandisi Sijapata Athuman wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira(Dawasa) ambao ndio watekelezaji wa mradi huo amesema sasa wakazi wa Buza watakuwa na…