Operesheni ya pamoja ya nchi tatu dhidi ya mbabe wa kivita wa Afrika
Katika operesheni ya pamoja, nchi tatu za Afrika zililenga na kuharibu kambi za Lord’s Resistance Army (LRA) zinazoongozwa na Joseph Kony, mmoja wa wababe wa kivita wanaosakwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, likinukuu shirika la habari la AFP, jeshi la Uganda linalojulikana kama “People’s Defence Forces”…
DRC kupokea chanjo ya Mpox wiki ijayo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ina matumaini ya kupokea dozi ya kwanza ya chanjo ya Mpox wiki ijayo. Ni baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza jana Jumatatu, Agosti 19, kwamba nchi zilizoathiriwa na janga la Mpox zinapaswa kuanzisha mipango ya kutoa chanjo katika maeneo ambayo yamathiriwa zaidi na ugonjwa huo. Congo DR imeripoti kesi 16,700…
Ukraine yapoteza njama barani Afrika
Ukraine inapaswa kuwa makini kutorudia makosa ya Vita Baridi. Mnamo Agosti 5, serikali ya Mali ilitangaza uamuzi wake wa kukata uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine, ikitoa mfano wa afisa wa Ukraine kukiri kwa majigambo kwamba Kyiv iliwapa waasi wa Mali akili muhimu kwa shambulio la waasi ambalo liliua mamluki wengi wa Wagner Group wa Urusi…
UK ilihusika katika kuwapa mafunzo askari wa Ukraine kabla ya kushambulia eneo la Kursk la Russia
Gazeti la Times linalochapishwa Uingereza limefichua kuwa wanajeshi wa Ukraine walioshiriki katika uvamizi wa vikosi vya Kiev katika mkoa wa Kursk wa Russia, walipewa mafunzo na wataalamu wa kijeshi wa Uingereza katika kipindi cha wiki chache kabla ya kufanyika shambulio hilo la kushtukiza. Mnamo Agosti 6, vikosi vya Ukraine vilianzisha shambulio kubwa zaidi dhidi ya…
Rais wa Zimbabwe atoa mwito wa kufanyika juhudi za kuhifadhi historia ya Afrika
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana Jumapili alizitaka nchi za Afrika kuhakikisha kwamba historia ya bara hilo imeandikwa kwa usahihi na kulindwa ili kuzuia dosari za kihistoria. Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Meidani ya Ukombozi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Jumba la Makumbusho ya Ukombozi…
Algeria: Jeshi letu liko tayari kusaidia Gaza
Rais wa Algeria, Abdel Majid Taboun, alitangaza kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kuwasaidia watu wa Gaza na kwamba wakati wowote mpaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza utakapofunguliwa, litakuwa na uwezo wa kujenga hospitali 3 ndani ya siku 20. Wakati wa kampeni zake za uchaguzi katika mkusanyiko wa wafuasi wake katika jimbo…
The Independent: 92% ya Waislamu wa Uingereza hawana amani
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na kuchapishwa na gazeti la The Independent la Uingereza unaonyesha kuwa, asilimia 92 ya Waislamu wa nchi hiyo hawahisi kuwa na amani. Uchunguzi huo wa maoni unaeleza kuwa, asilimiia 92 ya Waislamu wanahisi kutokuwa amani kabisa ya kuishi nchini Uingereza. Kulingana na uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika la Muslim Census…
Mazuwari waendelea kumiminika Karbala kwa ajili ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as)
Mazuwari kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Iraq na maeneo mengine ya dunia wameendelea kumiminika katika mji wa Karbala kwa ajili ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as). Mji wa Karbala umeanza kushuhudia wimbi kubwa la umati wa watu wanaoingia mjini humo wengine wakitembea kwa miguu kutoka miji mbalimbali kama ya basra na Najaf kuelekea…