Huyu ndiye Ismail Haniyeh, Kiongozi Mkuu wa Kisiasa wa HAMAS aliyeuawa shahidi Tehran
Jumanne usku ya tarehe 30 Julai 2024, Ismail Haniyeh Kiongozi wa Tawi la Kisiasa la Harakati ya HAMAS ameuawa shahidi akiwa na mlinzi wake mmoja hapa Tehran. Ufuatao hapa chini ni wasifu kwa muhtasari wa maisha yake. Ismail Haniyeh alizaliwa mwaka 1962 katika kambi moja ya wakimbizi ya Ukanda wa Ghaza. Ukata na njaa iliyotokana…
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel-Fattah al Burhan anusurika katika jaribio la mauaji
Jeshi la Sudan limetangaza kuwa kamanda wake mkuu, Jenerali Abdel-Fattah al Burhan amenusurika katika shambulio la ndege mbili sisizo na rubani (droni) katika hafla ya wahitimu wa jeshi. Watu watano wameuawa katika hujuma hiyo ya droni mashariki mwa Sudan. Jeshi la Sudan limeeleza katika taarifa yake kuwa shambulio hilo la droni mbili limetokea katika mji…
Afisa wa zamani wa CIA: Mauaji ya Haniyeh yalifanywa kwa ujuzi na msaada wa Amerika na Uingereza
Afisa huyo mstaafu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) akielezea juu ya kuuawa shahidi Ismail Haniyeh, kiongozi wa kisiasa wa Hamas, kuwa ni kuvuka mstari mwekundu na kuongeza kuwa mauaji haya yalitekelezwa kwa ujuzi na uungaji mkono wa Uingereza na Marekani. Larry Johnson alisisitiza katika sehemu nyingine ya mahojiano haya: “Nasema hivi kwa sababu…
Rwanda na DRC zakubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa Congo
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa DRC kuanzia Agosti 4 ya mwezi ujao katika mkutano uliofanyika mjini Luanda Angola. Hayo yametangazwa na ofisi ya rais wa Angola, nchi ambayo imekuwa mpatanishi katika duru kadhaa za mazungumzo ya kumaliza uhasama kati ya…
Maoni ya Ikulu ya White House kuhusiana na mauaji ya Ismail Haniyeh
Msemaji wa Ikulu ya Marekani ametangaza kuwa taasisi hiyo iliarifiwa kuhusu kuuawa shahidi Ismail Haniyeh, kiongozi wa kisiasa wa Hamas mjini Tehran, lakini ikakataa kutoa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA kutoka CNN siku ya Jumatano, baada ya kuuawa Ismail Haniyeh na kuuawa shahidi, msemaji wa Ikulu ya White House alisema kuwa Ikulu…
Ismail Haniyeh na mmoja wa walinzi wake wauawa mjini Tehran
Katika tangazo la IRGC Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, na mmoja wa walinzi wake wameuawa kishahidi baada ya shambulio katika makazi yao mjini Tehran. Uhusiano wa umma wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulitangaza katika tangazo: Mheshimiwa Dk. Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, na mmoja…
Algeria imemrudisha nyumbani balozi wake kutoka Ufaransa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria ilimwita balozi wake kutoka Ufaransa kupinga hatua ya Ufaransa kuingilia kati kuhusu mpango wa kujitawala wa Sahara Magharibi. Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA ya Jumanne iliyonukuliwa na Al-Nashrah, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Algeria ilitangaza kuwa baada ya Ufaransa kutangaza kuunga mkono mpango wa Maghreb wa…
Baraza Kuu la Waislamu Kenya launga mkono mazungumzo ya kitaifa
Baraza Kuu la Waislamu Nchini Kenya (SUPKEM) limeunga mkono mazungumzo kuhusu masuala ambayo yameibuliwa vijana wanaofanya maandamano dhidi ya serikakli ya Rais William Ruto maarufu kama na Gen Z ili kukomesha zogo la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa nchini humo. Mwenyekiti wa Supkem, Hassan Ole Naado, amesema kuwa baraza hilo linataka muafaka wa kisiasa ufikiwe ili kuyashughulikia…