
Taqwa pamoja na marafiki, ndugu wanaopotosha katika njia sahihi: Ustadh Syed Jawad Naqvi
Hujjatul Islam Ustadh Syed Jawad Naqvi (Kiongozi mkuu Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa na: Masjid Baitul ul Ateeq Lahore – Pakistan Khutba ya Ijumaa – 29 Novemba 2024 Khutba ya 1: Taqwa pamoja na marafiki, ndugu wanaopotosha katika njia sahihi Taqwa ina umuhimu mkubwa wakati wa kuamiliana na watu wengine, kwani mahusiano haya ni…

Nigeria yaripoti vifo 15,000 vinavyohusiana na UKIMWI kila mwaka
Nigeria inarekodi takriban vifo 15,000 vinavyohusiana na Ugonjwa wa Ukimwi kila mwaka licha ya juhudi za serikali za kukabiliana na kuenea ugonjwa huo hatari katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika. Temitope Ilori, mkuu wa Shirika la Taifa la Kudhibiti Ukimwi nchini Nigeria (NACA) amewaambia waandishi wa habari wakati wa shughuli ya uhamasishaji…

Kwa mara nyingine Ronald Lamola ataka kukomeshwa vita mara moja Ghaza
Kwa mara nyingine tena, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ametaka kukomeshwa vita mara moja katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina na kufikishiwa misaada wakazi wa eneo hilo haraka iwezekanavyo. Ronald Lamola alitoa mwito huo jana mjini Cairo Misri baada ya mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Badr…

Putin: Tuko tayari kusimamisha vita nchini Ukraine
Ikulu ya Russia imetangaza habari ya kufanyika mazungumzo ya simu baina ya Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz ambapo Putin amesema kuwa nchi yake iko tayari kuanzisha mazungumzo ya kusimamisha vita nchini Ukraine. Kwa mujibu wa shirika la habari la TASS la Russia, rais wa nchi hiyo na kansela…

Ghorofa laporomoka Kariakoo Dar e Salaam, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha
Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya jengo la ghorofa lililoko Kariakoo jijini Dar es Salaam Tanzania kuporomoka. Taarifa zaidi zinasema kuwa, jengo moja la biashara limeporomoka asubuhi ya leo katika mtaa wa Kongo, Kariakoo Jijini Dar es Saalam na kwamba, juhudi za uoakoji zinaendelea. Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walipokea taarifa…

MSF yaanza upya kutoa huduma kwa wananchi waliokumbwa na njaa magharibi mwa Sudan
Shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa, limeanza tena kutoa huduma katika kambi ya wakimbizi ya mji wa El Fasher wa Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan kutokana na watu katika kambi hiyo kukumbwa na njaa kali na magonjwa ya kuambukiza. Kundi hilo limesema hayo katika mtandao wa kijamii wa…

UN yatoa mwito wa kupunguzwa mvutano wa baada ya uchaguzi nchini Msumbiji
Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka mvutano na machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Msumbiji ambayo yameshapelekea watu 20 kupoteza maisha huku usalama ukizidi kudorora. Volker Turk ametoa mwito huo kwenye taarifa maalumu akisema: “Nimekuwa nikifuatilia matukio ya Msumbiji ya baada ya uchaguzi kwa wasiwasi mkubwa, na…

Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Duniani watoa wito wa kusaidiwa taifa la Palestina
Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu Duniani umezitaka nchi za Kiislamu kuchukua hatua ya kulisaidia taifa la Palestina dhidi ya jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Sheikh Ali al-Qaradaghi, Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Duniani (IUMS) jana Alkhamisi aliashiria jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kuutaka…