Cuba kujiunga rasmi kwenye kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel ICJ
Cuba imetangaza kutuma ombi la kujiunga kwenye kesi ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai dhidi ya binadamu katika Ukanda wa Gaza. Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba imesema katika taarifa ya jana Ijumaa kuwa, Havana itajiunga rasmi kwenye kesi ya Afrika…
Mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa: UAE imehusika katika kuendelea kwa vita
Mwakilishi wa serikali ya Sudan katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alisema kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu ndio sababu ya kuendelea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kwa kuunga mkono wanamgambo wa “majibu ya haraka”. “Idris Mohammad”, mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, alisema kuwa Umoja wa Falme za…
WFP yapata dola milioni 37 za kusaidia wakimbizi nchini Kenya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lmetangaza kwamba limepata mchango wa dola milioni 37 za Kimarekani kama msaada wa chakula na lishe kwa wakimbizi walioko nchini Kenya, msaada ambao utaliwezesha shirika hilo kuongeza mgao kwa wakimbizi walioko hatarini zaidi katika kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakma hadi mwezi Disemba…
“siri” na mpango wa Netanyahu kusalia madarakani yafichuka
Gazeti la Israel la Ma’ariv lilichapisha mahojiano yake na mwanasiasa wa Israel kuhusu mpango wa siri wa Benjamin Netanyahu wa kusalia madarakani kwa kuahirisha uchaguzi wa 2026. Katika tovuti yake, Gazeti hili lilichapisha mahojiano yake pamoja na mwanasiasa wa Israel mwenye mafungamano na chama cha Likud ambaye hapo awali alifanya kazi na waziri mkuu anayekalia…
Afrophobia tishio kwa ndoto ya Afrika
Kuna haja ya kuikumbatia tena ndoto ya umoja wa Afrika na kudai uhuru wa kusafiri kwa Waafrika wote ndani ya bara hili. Akiongea katika Jukwaa la Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika mjini Kigali, Rwanda, tajiri mkubwa zaidi barani Afrika, na bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, alilalamika kwamba anakabiliwa na vizuizi vingi zaidi vya kuzunguka Afrika hata…
Kwa nini Washington ilighairi mkutano wake na Tel Aviv kuhusu Iran?
Tovuti ya Marekani ya “Axios” ilitangaza kuhairishwa kwa mkutano muhimu wa maafisa wa ngazi za juu wa Washington na maafisa wa utawala wa Kizayuni kuhusiana na Iran. Tovuti ya Axios ilinukuu maafisa wa Marekani wakisema: Kufuatia shambulio la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu dhidi ya Rais wa Marekani Joe Biden kuhusu mauzo ya silaha,…
Njaa ni tishio kubwa kwa wakimbizi wa Sudan nchini Chad
Kwa Mujibu wa mashirika ya misaada; Njaa iliyokithiri nchini Sudan yasababisha maelfu ya raia kutoka mjini Darfur kukimbilia nchini Chad. Adre, Chad – ikiwa chini ya jua kali, ndio sehemu ambayo Awatef Adam Mohamed amepata kimbilio nje ya mpaka wa jangwa kati ya Sudan na Chad. Aliwasili Juni tarehe 8, na kuungana pamoja na makumi…
Putin: Njama za Magharibi za kujaribu kuidhibiti Russia zimefeli
Rais Vladimir Putin wa Russia amesisitiza kuwa, njama zote za madola ya Magharibi za kutaka kuifanya Moscow itengwe kimataifa zimefeli. Hayo yameripotiwa na shirika la habari la FARS ambalo limemnukuu Putin akisema: “Si muhimu kwetu wamefanya njama kubwa kiasi gani, lililo muhimu kwetu ni kwamba njama zao zote za kutaka kuifanya Russia itengwe, zimefeli.” Rais…