Habari

Kenya yawawinda wanaoeneza chuki kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9

Kenya yawawinda wanaoeneza chuki kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9

Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa ya Kenya (NCIC), inachunguza watu 51 kwa tuhuma za kusambaza matamshi ya chuki huku kaunti sita zikikihofiwa kukumbwa na vurugu za kisiasa katika kipindi hiki nyeti cha kampeni kali za kuwapigia debe wanasia wanaowania kiti cha rais wa nchi hiyo. Mwenyekiti wa NCIC, Samuel Kobia, amesema watu 36…

Umoja wa Mataifa: Udhalilishaji unaofanywa na serikali ya Sudan Kusini ni sawa na jinai za kivita

Umoja wa Mataifa: Udhalilishaji unaofanywa na serikali ya Sudan Kusini ni sawa na jinai za kivita

UN imesema kuwa viongozi na maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wamekiuka haki za binadamu nchini humo; vitendo vilivyotajwa kuwa ni sawa na jinai za kivita. Ukiukaji huo wa haki za binadamu umewakumba pia watoto wa Sudan Kusini. Nchi hiyo changa zaidi duniani imekuwa ikishuhudia mapigano na ukosefu wa amani tangu ipate uhuru mwaka 2011;…

Kwa mara ya Kwanza Uchina yaripoti vifo vya kwanza kutokana virusi vya Covid-19 baada ya kipindi cha mwaka mmoja

Kwa mara ya Kwanza Uchina yaripoti vifo vya kwanza kutokana virusi vya Covid-19 baada ya kipindi cha mwaka mmoja

Mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa omicron bado unaendelea katika baadhi ya majimbo ya China, huku idadi ya wahasiriwa wa corona nchini ikifikia 4,638, kulingana na takwimu zilizorekodiwa. Kulingana na Shirika la Habari la Associated Press, maafisa wa afya wa kitaifa wa China mnamo siku ya Jumamosi waliripoti vifo viwili vilivyotokana na virusi vya Covid-19, ikiwa…

Tarehe 15 Shaaban Hijiria Qamaria ni kumbukumbu ya kuzaliwa mwokozi wa ulimwengu, Imam Mahdi –Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake (ATF)

Tarehe 15 Shaaban Hijiria Qamaria ni kumbukumbu ya kuzaliwa mwokozi wa ulimwengu, Imam Mahdi –Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake (ATF)

Nuru ya umaanawi ya uwepo wa Imam Mahdi ATF imeenea hata katika wakati huu wa “ghaiba” au kutokuwepo mtukufu huyo machoni mwa walimwengu. Kabla ya kumuumba mwanadamu, Mwenyezi Mungu aliwaambia Malaika wake: ‘Na pale Mola wako alipowaambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (al-Baqarah:30). Khalifa wa kwanza alikuwa Nabii Adam (as) na baada yake wakaja Manabii na…

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameilaumu NATO kwa vita vya Russia nchini Ukraine

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameilaumu NATO kwa vita vya Russia nchini Ukraine

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameilaumu NATO kwa vita vya Ukraine na kusema kuwa atapinga wito wa kuilaani Russia. Matamshi haya ya Ramaphosa yanatia shaka iwapo atakubaliwa na Ukraine au nchi za Magharibi kama mpatanishi katika mzozo huo. Ramaphosa ambaye alikuwa akizungumza bungeni, amesema: “Vita hivyo vingeweza kuepukika kama NATO ingezingatia maonyo kutoka kwa viongozi…

Raila Odinga: Sitamwacha Uhuru Kenyatta iwapo nitashinda uchaguzi wa rais wa Agosti 9

Raila Odinga: Sitamwacha Uhuru Kenyatta iwapo nitashinda uchaguzi wa rais wa Agosti 9

Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, amesema kuwa hatamwacha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti 9, 2022. Raila amesema kuwa Rais Kenyatta amekuwa nguzo muhimu katika utulivu wa taifa na uchumi na kwamba yeyote atakayeshinda hastahili kumtelekeza. Amesema iwapo atashinda uchaguzi ujao ataendeleza uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta na…

Ufaransa yafunga Msikiti mwingine kwa madai ya kuruhusu mawaidha yasiyokubalika kiserikali

Ufaransa yafunga Msikiti mwingine kwa madai ya kuruhusu mawaidha yasiyokubalika kiserikali

Ikiwa ni katika kuendeleza chuki na uadui wake dhidi ya Uislamu, serikali ya Ufaransa imefunga Msikiti mwingine kwa muda wa miezi sita kwa madai ya kuruhusu mawaidha yasiyokubaliwa na serikali ya Paris. Kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu, mkuu wa mkoa wa Bordeaux ametoa taarifa ya kuvunjwa Msikiti wa al Farouk ulioko kwenye eneo la Pessac…

Medvedev: Urusi yawaweka maadui zake sehemu wanayostahiki, miongoni mwao Marekani

Medvedev: Urusi yawaweka maadui zake sehemu wanayostahiki, miongoni mwao Marekani

Naibu Katibu wa Baraza la Usalama la Russia amesema kuwa Marekani imezusha hofu ya kuchukiza nchini Urusi katika jaribio la kuipigia magoti Moscow na kuisambaratisha. Alisema kuwa Urusi ina uwezo wa kuwaweka maadui wake wote wabaya mahali pake. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, Dmitry Medvedev alisema siku ya…