Habari

Rais Volodymyr Zelenskyy : Nchi za Magharibi hazina hata uwezo wa kulinda wananchi wao

Rais Volodymyr Zelenskyy : Nchi za Magharibi hazina hata uwezo wa kulinda wananchi wao

Zelenskyy alisema hayo siku ya Ijumaa katika hotuba yake maalumu na kuongeza kuwa, hivi sasa mtu yeyote atakayeuawa nchini Ukraine, basi nchi za Magharibi zinabeba dhima ya kifo chake. Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amehamakishwa mno na uamuzi wa Jeshi la Nchi za Magharibi NATO kukataa ombi lake la kutangaza eneo lililo marufuku kupaa ndege…

Moto mkubwa waripotiwa katika kituo kikubwa zaidi cha nyuklia cha Ukraine

Moto mkubwa waripotiwa katika kituo kikubwa zaidi cha nyuklia cha Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ukraine mapema leo Ijumaa amesema kuwa moto mkubwa umetokea katika kituo kikubwa zaidi cha nyuklia cha nchi hiyo cha Zaporizhzhia. Dmytro Kuleba amedai kuwa moto huo umetokana na mashambulizi ya Jeshi la Russia dhidi ya kituo hicho. Zaporizhzhia ndicho kituo kikubwa zaidi cha nishati ya nyuklia nchini…

Bin Salman: Tuna matumaini ya kuendelezwa mazungumzo na Iran

Bin Salman: Tuna matumaini ya kuendelezwa mazungumzo na Iran

Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ameeleza matumaini kuwa mazungumzo kati ya Iran na Saudi Arabia yatafikia hatua ambayo itakuwa nzuri kwa pande zote mbili na kutengeneza mustakabali mzuri kwa nchi zote mbili. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran, IRNA, Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman amesema kwamba Riyadh itaendelea na mazungumzo yake…

Mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Yemen Yaendelea Saudia ikiwa mhusika mkuu

Mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Yemen Yaendelea Saudia ikiwa mhusika mkuu

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudia huko Yemen jana ziliendelea kuyashambulia maeneo mbalimbali ya raia Waisalmu katika mikoa tofauti ya Yemen. Televisheni ya al Masira imeripoti kuwa, ndege za kivita za muungano vamizi huko Yemen zinazoongozwa na Saudi Arabia jana zilishambulia maeneo ya raia katika mikoa ya Saada…

Hujjatul Islam Haj Ali Akbari : Marekani imehusika na yanayoendelea Ukraine

Hujjatul Islam Haj Ali Akbari : Marekani imehusika na yanayoendelea Ukraine

Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehrah amekosoa vikali mienendo ghalati ya Marekani katika medani ya kimataifa na kusisitiza kuwa, US ni nembo ya ujahili mamboleo. Hujjatul Islam Haj Ali Akbari ameashiria matukio ya Ukraine na operesheni maalumu ya kijeshi ya Russia ndani ya ardhi ya nchi hiyo ya Ulaya na kueleza…

Iran: Azimio la UNSC kuhusu Yemen lina taathira hasi kwa mwenendo wa kutafuta amani

Iran: Azimio la UNSC kuhusu Yemen lina taathira hasi kwa mwenendo wa kutafuta amani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa Yemen na lugha iliyotumika katika azimio hilo vitakuwa na taathira hasi kwa mwenendo wa amani na kupanua zaidi ufa uliopo baina ya misimamo ya pande mbili zinazopigana. Saeed Khatibzadeh ameongeza kuwa, inasikitisha kuona…

Wapalestina 190 watiwa mbaroni na askari wa Israel ndani ya muda wa mwezi mmoja

Wapalestina 190 watiwa mbaroni na askari wa Israel ndani ya muda wa mwezi mmoja

Jumuiya ya Ulaya ya kutetea na kuunga mkono Quds tukufu (Jerusalem) imetangaza kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja, askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamevamia mji huo wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na kuwatia nguvuni Wapalestina zaidi ya 190 wakazi wa mji huo. Hujuma na mashambulio ya askari wa utawala wa Kizayuni…

Moscow: Ipo hatari ya makabiliano ya moja kwa moja kati ya Urusi na NATO

Moscow: Ipo hatari ya makabiliano ya moja kwa moja kati ya Urusi na NATO

Kuna hatari ya makabiliano ya moja kwa moja kati ya Urusi na NATO, lakini Moscow inatafuta kutatua suala hilo kwa njia za kidiplomasia, alisema naibu waziri wa mambo ya nje. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alisema Jumatano mchana, saa za…