Mataifa ya Sahel yafanya luteka ya kijeshi Niger
Mataifa matano ya Kanda ya Sahel yanafanya luteka ya kijeshi magharibi mwa Niger, ikiwa ni mara ya kwanza kwa shughuli ya aina hiyo kufanywa katika eneo linalokumbwa na machafuko ya makundi ya itikadi kali. Eneo la Sahel limegubikwa kwa miaka mingi na waasi wenye mafungamano na makundi ya waasi. Wizara ya ulinzi ya Niger imesema…
Kaimu Rais wa Iran: Tunafungamana na mkakati wetu wa kuimarisha ushirikiano na nchi za Kiislamu
Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili linafungamana kikamilifu na stratejia na mkakati wake wa kuimarisha ushirikiano wake na mataifa ya Kiislamu. Muhammad Mokhber amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran Spika wa Bunge la Mali. Huku akiishukuru serikali na wananchi wa Mali kwa kuonyesha mshikamano wao na serikali…
Rais wa Tanzania atia saini kitabu chenye ujumbe wa kuomboleza kifo cha kishahidi cha Ayatollah Raisi
Bi Samia Saluho Hassan, Rais wa Tanzania, alihudhuria Ubalozi wa Iran jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa; Alitia saini kitabu cha kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Ayatullah Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutoa salamu za rambirambi kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu; Serikali na watu wa…
Waislamu wa Tanzania wamuomboleza Sayyid Ebrahim Raisi
Waislamu nchini Tanzania wameshiriki katika hafla ya kuwakumbuka na kuwaenzi viongozii wa Iran walioaga dunia hivi karibuni akiwemo Rais Ebrahim Raisi. Waislamu wa Tanzania wamefanya kumbukumbu ya maombolezo ya kumuenzi Rais wa Iran aliyeaga dunia Ebrahim Rais pamoja na maafisa wengine aliokuwa ameambatana nao akiwemo waziri wake wa mashauri ya kigeni Hussein Amir-Abdollahian. Maombolezo hayo…
Polisi wa Uingereza wamewakamata waandamanaji wanaounga mkono Palestina
Maandamano ya wanafunzi wa Marekani na Ulaya ya kusitisha uchokozi wa utawala ghasibu wa Israel katika ukanda wa Ghaza na kukata uhusiano wa kielimu na vyuo vikuu vya utawala huo ghasibu kwa mabavu yanaendelea. Licha ya mapigano hayo na kukamatwa kwao, hali iliyopelekea kupigwa marufuku kuendelea na masomo, wanafunzi hao walisisitiza kuwa maandamano hayo yameongeza…
Zuma: Nitapigania haki yangu ya kuwania ubunge Afrika Kusini
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameapa kupigania kile alichokiita ‘haki yake’ ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika wiki ijayo. Jumatatu iliyopita, Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini ilitoa hukumu kwamba Zuma hastahiki kugombea katika uchaguzi huo, ikisisitiza kuwa hana sifa za kuwa mgombea kwenye zoezi hilo la kidemokrasia. Kwenye video iliyotumwa kwenye jukwaa…
Waziri wa Israel: Mashambulizi ya Iran yameharibu kambi mbili kuu za jeshi; akejeli taarifa za Israel kushambulia Iran
Waziri wa Usalama wa Ndani ya serikali ya Benjamin Netayahu amekiri kwamba shambulio la kulipiza kisasi la Iran dhidi ya Israel limesababisha hasara kubwa za kijeshi kwa utawala wa Kizayuni na wakati huo huo ameziita taarifa zilizodai kuwa utawala wa Kizayuni umefanya shambulizi ndani ya Iran leo Ijumaa kuwa ni istihzai. Mkanda wa video ulioenea…
Biden anaiongeza Kenya katika orodha ya Washington ya washirika wakuu wasio wa NATO
Katika mkutano wa pamoja wa wanahabari na Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Marekani siku ya Alhamisi, Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi kuongeza nchi hiyo katika orodha ya washirika wakuu wa Marekani wasio wa NATO. Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA Ijumaa asubuhi, iliyonukuliwa na Al Jazeera, Biden alisema katika mkutano huu…