Jeshi la Yemeni na Kamati za Wananchi zasonga mbele katika mji uliopokaribu na mpaka wa Harz
Faraan : Vyombo vya habari vya Yemen viliripoti kusongea karibu kwa vikosi vya jeshi la Yemen na Kamati za Wananchi katika mji wa Harz mkoani Hajjah kwenye mpaka wa Saudia. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Fars, vyanzo vya Yemen viliripoti kukaribia kwa vikosi vya jeshi la Yemen na Kamati za Wananchi…
Nablos: Wapalestima 165 wajeruhiwa na wanajeshi wa Israel
Shirika la Hilal Nyekundu la Palestina limeripoti kuwa, Wapalestina wasiopungua 165 wamejeruiwa na wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Nablos, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan jana Ijumaa pekee. Kila siku Wazayuni wanaua na kujeruhiwa makumi ya Wapalestina pamoja na kuvunja nyumba zao, kuharibu mashamba yao na kuteka maeneo yao. Mamia…
Utawala wa Kizayuni ulitengua ndege isiyo na rubani katika mpaka wa Lebanon
Vyombo vya habari vya Kizayuni vinathibitisha kuwa wanamapambano wa Kizayuni waliifyatulia kimakosa ndege ya utawala isiyo na rubani kwenye mpaka na Lebanon na kuitengua. Faraan : vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni leo Jumapili vimesema: Jeshi la utawala huo wa Kizayuni lilishambulia kimakosa ndege ya UAV kwenye mpaka wa Lebanon na kuiangusha kutokana na…
Masuala muhimu katika mazungumzo ya “Sayyid Hassan Nasrallah” na Televisheni ya Al-Alam
Maneno ya Sayed Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Alam siku ya Jumanne, mazungumzo yake yalikuwa mazuri mno kiasi kwamba wale wenye kutafuta ukweli kuhusu maendeleo ya Lebanon na eneo hilo watafaidika zaidi na matamshi hayo. Wasikilizaji wa mahojiano ya “Sayed Hassan Nasrullah” na…
Iran yaadhimisha miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Leo Ijumaa tarehe 22 Bahman, sawa na tarehe 11 Februari, wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanaadhimisha sherehe za miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini. Katika sherehe hizo mamilioni ya wananchi wa taifa hili watamiminika mabarabarani katika maandamano ya amani ya kumbukumbu ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, ambapo kwa mara…
Wapalestina watoa shukrani kwa AU kwa kuitoa Israel kwenye umoja wa Afrika
Harakati za muqawama wa Palestina za Hamas na Jihad al Islami zimeushukuru Umoja wa Afrika (AU) kwa kuutimua utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye umoja huo na kusema kuwa, hatua hiyo ni pigo kwa zile nchi zinazotangaza uhusiano wa kawaida na utawala huo katili. Wakuu wa Umoja wa Afrika (AU), jana Jumapili walisimamisha nafasi ya mwanachama…
Takriban Wayemen elfu nne ni wahanga wa mabomu ya vishada ya Saudia na washirika wake
Mabomu ya vishada ya muungano vamizi katika vita vya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia yanayovurumishwa kwa wananchi wasio na hatia hadi kufikia mwaka jana wa 2021 yameuwa raia karibu elfu nne wa nchi hiyo. Taasisi za Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) zimetahadharisha mara…
Al Houthi: Uamuzi wa AU dhidi ya Israel ni pigo kubwa kwa wanaopatana na Wazayuni
Mjumbe mmoja mwandamizi wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, hatua ya Umoja wa Afrika (AU) ya kuutimua utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye umoja huo ni pigo kubwa kwa wale wanaojipendekeza kwa utawala huo dhalimu. Muhammad al Houthi amesema kuwa, uamuzi wa Umoja wa Afrika ni pigo kubwa pia kwa zile nchi…