Yemen yaua makumi ya mamluki wa Saudia kupitia kombora zito
Makumi ya mamluki wa muungano vamizi wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia wameangamizwa baada ya vikosi vya jeshi la Yemen kuwavurumishia kombora la balestiki lililopiga kambi ya mamkuli hao katika mkoa wa Ma’rib, katikati mwa Yemen. Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kombora hilo limelenga mkusanyiko wa mamluki wa serikali iliyojiuzulu…
Iran: Mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa kukiwa na wavamizi wa kigeni
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani ukiukaji wa mamlaka ya kitaifa ya kijitawala Syria ambao unatekelezwa na askari vamizi wa kigeni na magaidi na kusema, mgogoro wa muda mrefu wa nchi hiyo hauwezi kutatuliwa iwapo kutaendelea kuwepo nchini humo wavamizi wa kigeni. Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Majid Takht-Ravanchi aliyasema hayo Jumatano katika…
Maandamano ya nchi nzima kupinga mauaji ya kidhulma ya watu wa Yemen baada ya sala ya Ijumaa wiki hii
Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu sambamba na kulaani vikali mauaji ya kikatili ya wananchi madhulumu wa Yemen yaliyofanywa na muungano wa Saudia na Imarati, limetoa taarifa na kulitolea wito taifa kubwa la Iran kushiriki katika maandamano dhidi ya jinai hizo. Kwa mujibu wa kundi la kisiasa la Shirika la Habari la Faraan, Baraza…
Rais Raisi: Uhusiano wa Iran na Azerbaijan unatokana na imani za wananchi kwa misingi yao ya pamoja ya kidini
Rais Ebrahim Raisi amesema, uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan unatokana na itikadi na imani za watu wa nchi mbili kwa misingi yao ya pamoja ya kidini. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Azerbaijan Zakir Hasanov na akasisitiza…
Mufti wa Lebanon: Moto wa vita vya Yemen utachoma miji mikuu ya nchi za Kiarabu
Mufti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon amesema kuwa, iwapo moto wa vita vya Yemen hautazimwa, utachoma pia miji mikuu ya nchi za Kiarabu. Sheikh Ahmed Qabalan ambaye alikuwa akizungumzia mapigano yaliyopamba moto zaidi huko Yemen ameziambia serikali za nchi za Kiarabu kwamba: “Zimeni moto wa Yemen kabla ya miji mikuu ya Waarabu haijateketea kwa…
Sauti ya mlipuko yasikika ndani ya mji mkuu wa Iraq – Baghdad
Duru za habari zimearifu kuwa sauti ya mlipuko imesikika mapema leo magharibi mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq. Sauti ya mlipuko imesikika leo magharibi mwa mji mkuu wa Iraq na karibu na jela ya Abu Ghureib. Hadi tunaingia matangazoni hakuna taarifa yoyote iliyotufikia kuhusu maafa yaliyosababishwa na mlipuko huo. Duru za habari kutoka Iraq aidha…
Katibu Mkuu wa UN alaani “janga la mapinduzi” baada ya Kabore kupinduliwa Burkina Faso
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani kile alichokiita “janga la mapinduzi” ambalo ulimwengu unashuhudia, akieleza kuwa anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa matukio ya sasa nchini Burkina Faso. Guterres ameeleza wasiwasi wake hasa kuhusu hatima na usalama wa Rais Roch Marc Christian Kabore wa Burkina Faso kufuatia mapinduzi yaliyofanywa na vikosi vya wanajeshi juzi Januari 23….
Moscow: Utumaji wa silaha kwa nchi ya Ukraine ni sababu ya vifo vya raia wakawaida
Mjumbe wa Urusi katika Umoja wa Mataifa alisema Jumanne kwamba hatua ya baadhi ya nchi za magharibi ya kutuma silaha nchini Ukraine ni jambo litakalosababisha vifo vya raia wa kawaida waliopo mashariki mwa nchi hiyo. Faraan: Imeripotiwa kwamba; “Mwakilishi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Bw. Gennady Kozmin, alisema wakati wa mkutano wa Baraza la…