Baqeri Kani: Hatua kadhaa katika suala la uondoaji vikwazo
Ali Bagheri Kani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA amesema; kutokana na mazungumzo ya karibuni mjini Vienna, zimepigwa hatua nzuri katika suala la uondoaji vikwazo. Bw. Kani katika mazungumzo ya Vienna amesema kuwa; katika kipindi…
Kuondolewa vikwazo Iran; siri ya mafanikio ya mazungumzo ya Vienna
Mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 4+1 linaloundwa na mataifa ya Russia, China, Uingereza, Ufaransa pamoja Ujerumani yaliendelea tena leo huko Vienna Austria maudhui kuu ikiwa ni suala la kuondolewa vikwazo na kutilia mkazo mapendekezo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu masuala mawili muhimu, yaani uhakika kwamba vikwazo vimeondolewa na dhamana yake….
Waziri Mkuu wa Lebanon: Hizbullah ina haki ya kufanya shughuli zake sawa kabisa na vyama vingine vya siasa
Waziri Mkuu wa Lebanon amesema kuwa harakati ya Hizbullah iko sawa kabisa na vyama vingine vya siasa vya nchini humo kwa kuwa ni chama cha siasa. Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika ikulu ya Waziri Mkuu, Najib Miqati Waziri Mkuu wa Lebanon amebainisha kuwa Lebanon inakabiliwa na matatizo na vitisho vingi na vikubwa; na hakuna njia…
Wanawake Afghanistan wapigwa marufuku kwenda safari ndefu bila wanaume
Maagizo hayo yametolewa siku ya Jumapili chini ya utawala wa Taliban ambapo shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights limesema marufuku hiyo inawafanya wanawake kujihisi kama wafungwa. Taliban imesema wanawake wa Afghanistan wanaotaka kusafiri umbali mrefu kwa barabara wanapaswa kupatiwa usafiri ikiwa tu wataandamana na ndugu zao wa kiume. . Maagizo hayo, yametolewa…
Shirika la Iran Khodro laanza tena kuunda magari Afrika
Shirika la Iran Khodro, ambalo ndilo shirika kubwa zaidi la kuunda magari Asia Magharibi, limetangaza kufungua tena kiwanda chake cha kuunda magari nchini Senegal. Shirika hilo la Iran litaanza kuunda magari aina ya Samand katika mji wa Thies, ambao ni wa pili kwa ukubwa Senegal na uko mbali wa kilimota 70 kutoka mji mkuu, Dakar….
Iran yasikitishwa na mauaji yaliyofanywa na magaidi Burkina Faso
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza kufungamana na familia za raia wa Burkina Faso ambao waliuawa katika hujuma ya kigaidi hivi karibuni. Katika taarifa leo Jumatatu, Saeed Khatibzadeh Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebainisha masikitiko yake makubwa kutokana na kupoteza maisha raia wa Burkina Faso katika hujuma…
Rais wa Somalia amfuta kazi Waziri Mkuu wake, mzozo wapamba moto
Rais wa Somalia amemfuta kazi Waziri Mkuu wake wakati huu wa kuendelea uchaguzi wa bunge na hivyo kuzusha mzozo mpya wa kisiasa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika. Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kusema kuwa, Rais Mohamed Abdullahi Farmaajo alichukua hatua hiyo jana Jumapili akimtuhumu Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble kuwa anahusika…
Jeshi la Yemen: Mkoa wa al Jawf umeshakombolewa kikamilifu
Msemaji wa Jeshi la Yemen amesema kuwa, mkoa wa al Jawf wa nchi hiyo umeshakombolewa kikamilifu kilichobakia ni mabaki ya hapa na pale tu ya wavamizi na mamluki wao. Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema hayo na kuongeza kuwa, vikosi vya ulinzi vya Yemen vimeendesha operesheni ya Fajr al Swahra (Mapambazuko ya Jangwani) na kufanikiwa kukomboa…