Makumi ya watu watekwa nyara jirani na Cabo Delgado nchini Msumbiji
Watu wenye silaha wamewateka nyara zaidi ya vijana 100 kutoka kijiji cha Naulala katika Mkoa wa Niassa kaskazini mwa Msumbiji. Mji wa Niassa unapakana na jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ambalo limekuwa katikak vita na makundi ya wanamgambo tangu Oktoba 2017. Taarifa zaidi zinasema kuwa, kundi la watu wenye silaha limewateka nyara vijana zaidi…
Shambulio jipya la waasi laua watu 33 Jamhuri ya Afrika ya Kati
Watu wapatao 33, wakiwemo wanajeshi wawili, wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa kwa wakati mmoja na watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi liitwalo 3R katika vijiji viwili vilivyoko kaskazini magharibi mwa mkoa wa Ouham-Pendé, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Faraan: Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa hiyo ni idadi kubwa zaidi ya watu…
Kiongozi: Wanaojidai watetezi wa haki za binadamu duniani walitoa msukumo kwa jinai za Saddam
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria jinai zilizofanywa na dikteta wa Iraq Saddam dhidi ya watu wa Iran na akasema: Saddam alikuwa akifanya jinai hizo kwa msukumo na uungaji mkono wa wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu duniani. Faraan: Tovuti ya habari ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo imetoa matini ya…
Watu 29, wakiwemo watoto, wapoteza maisha katika ajali ya boti Nigeria
Watu 29, wengi wakiwa ni watoto, wamepoteza maisha baada ya boti yao kuzama Nigeria katika Mto Bagwai jimboni Kano kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Msemaji wa kitengo cha zimamoto jimboni Kano Saminu Abdullahi amesema ajali hiyo ilitokea Jumanne usiku. Akizungumza Jumatano, Abdullahi amesema wamepata miili 29 na kuwaokoa abiria saba huku jitihada zikiendelea kwa ajili…
Al-Shabaab yashambulia askari wa Ethiopia, uwanja wa ndege Somalia
Kundi la kigaidi la al-Shabaab limeshambulia uwanja wa ndege na kambi ya kijeshi ya askari wa Ethiopia katika mji wa Baidoa, ulioko kusini magharibi mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Faraan: Duru za kiusalama zinaarifu kuwa, kwa akali askari mmoja ameuawa katika shambulio la kwanza lililolenga kambi ya jeshi la Ethiopia katika eneo la Suuqa…
Syria: Tunaunga mkono kuundwa nchi huru ya Palestina mji wake mkuu ukiwa ni Beitul-Muqaddas
Serikali ya Syria kwa mara nyingine tena imesisiitiza kuwa, inaunga mkono kuundwa nchi huru ya Palestina mji wake mkuu ukiwa ni Beitul-Muqaddas. Faraan: Sisitizo hilo limetolewa na Faisal Miqdad, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria katika ujumbe wake kwa masaba wa tarehe 29 Novemba ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Taifa…
Al Houthi: Maadui wanalenga kuitawala Yemen kupitia kuibua mifarakano
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuhusu njama za maadui za kuibua fitina na mifarakano kwa lengo la kueneza satwa yao katika nchi hiyo. Faraan: Amesisitiza kuwa, muungano wa kivita unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen unaendelea kutekeleza jinai hasa katika mji wa bandarani wa Hudaydah magharibi mwa nchi hiyo. Sayyid Abdul Malik…
OIC yamlaani rais wa Israel kwa kuingia Msikiti wa Ibrahim AS kinyume cha sheria
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani hatua ya Rais Isaac Herzog wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti wa Nabii Ibrahim AS katika mji wa Al Khalil au Hebron kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Faraan: Katika taarifa Jumatatu usiku, OIC imesema: “Kitendo hicho kimefanyika katika fremu…