
Hamas: Hali mbaya ya mateka wa Kipalestina katika jela za Israel itaibua vita
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislmu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, hali mbaya ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika korokoro za Israel utazucha cheche za mlipuko wa vita na utawala huo ghasibu. Abdul Latif al-Qanoua amesema harakati za mapambano za Palestina zinafuatilia kwa karibu hali ya mateka wa Kipalestina katika korokoro za Israel hususan…

Baraza Kuu la UN lapasisha maazimio 6 dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumanne ilipasisha maazimio sita dhidi ya utawala haramu wa Israel licha ya upinzani mkali wa wawakilishi wa Marekani, Canada na Israel. Faraan: Maazimio hayo ya Baraza Kuu la UN yamelaani ukiukaji wa kimfumo wa haki za binadamu za watu wa Palestina, utumiaji mabavu wa…

Wanafunzi 26 waaga dunia katika mkasa wa moto shuleni Niger
Wanafunzi wasiopungua 26 wameaga dunia katika mkasa wa moto ulioikumba shule moja nchini Niger. Shirika la habari la AFP limenukuu vyanzo vya habari vikisema kuwa, ajali hiyo ya moto imetokea usiku wa kuamkia leo katika shule moja iliyoko katika jimbo la Maradi, kusini mwa nchi. Chaibou Aboubacar, meya wa jiji la Maradi amesema kufikia sasa…

Israel imewafanyia ujasusi wafanyakazi wa asasi za kirai za Palestina
Shirika moja la kutetea haki za binadamu la Ulaya limefichua kuwa, programu ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni ya Pegasus imetumika kuwachunguza na kuwafuatilia wafanyakazi wa asasi za kiraia za Kipalestina, hususan zilizowekwa kwenye eti ya orodha ya ugaidi ya Tel Aviv. Faraan: Shirika la Front Line Defenders lenye makao yake Ireland lilisema jana katika…

Jeshi la Yemen latungua drone ya kijasusi ya Marekani ya ScanEagle huko Ma’rib
Jeshi la Yemen, likishirikiana na wapiganaji wa Kamati za Wananchi, limefanikiwa kutungua ndege isiyo na rubani (drone) ya Kimarekani ya ScanEagle ambayo ilikuwa na jeshi la Saudia kufanya ujasusi katika mkoa wa Ma’rib ambao umekuwa ukishuhudia mapigano makali hivi karibuni. Msemaji wa Jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree ametangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter…

Al khazali atilia shaka riwaya rasmi juu ya jaribo la mauaji ya Waziri Mkuu wa Iraq
Katibu Mkuu wa harakati ya Asaib Ahlul Haq nchini Iraq ametilia shaka riwaya na ripoti rasmi iliyotolewa na vyombo vya dola kuhusu shambulizi lililolenga makazi ya Waziri Mkuu wa nchi hio, Mustafa al Kadhimi mjini Baghdadi siku chache zilizopita Faraan: Qais al Khazali amesema kuna shaka katika riwaya rasmi inayosimilia jaribio la kuuliwa Waziri Mkuu,…

Jihad al Islami yatoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Kiongozi mmoja mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Jihad al Islami wa Palestina ametoa onyo kali kwa utawala wa Kizayuni wa Israel akitahadharisha kuwa, kama mateka mmoja tu wa Palestina atauawa shahidi, basi utawala huo utalipa jinai yake hiyo. Faraan: Kwa mujibu wa televisheni ya al Mayadeen, Khaled al Batsh alitoa onyo hilo…

Utawala dhalimu wa Israel wabomoa msikiti Ukingo wa Magharibi
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamebomoa msikiti wa Wapalestina katika mji wa Duma, kusini mwa eneo linalokaliwa kwa mabavu na utawala huo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Faraan: Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa katika jinai hiyo ya siku ya Alhamisi, buldoza za jeshi la utawala wa kikoloni wa Israel…