Risasi karibu na ubalozi wa Wazayuni nchini Sweden
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa mapema asubuhi ya leo, risasi zilifyatuliwa karibu na Ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Uswidi. Afisa wa Uhusiano wa Umma wa Idara ya Polisi ya Stockholm aliliambia gazeti la “Expressen” kwamba asubuhi ya leo polisi wa doria walisikia sauti ya milipuko mikubwa, ambayo inaonekana ilitoka kwa bunduki….
Waziri Mkuu Senegal akosoa uwepo wa kambi za kijeshi za Ufaransa nchini humo; asema huwenda zikafungwa
Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko, ameashiria uwezekano wa kufungwa kambi za kijeshi za Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Amesema hayo katika hotuba yake mbele ya vyombo vya habari ambayo pia imegusia sarafu ya CFA inayoungwa mkono na Ulaya, mikataba ya mafuta na gesi na kile kinachotajwa kuwa haki za LGBTQ (mabaradhuli) zinazopigiwa…
Kenya na Uganda zaafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta
Kenya na Uganda zimekubaliana kujenga kwa pamoja bomba la kusafirishia mafuta kutoka mjini Eldoret katika eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya hadi Uganda. Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo, serikali ya Kampala itaweza kuagiza moja kwa moja bidhaa za mafuta yaliyosafishwa kupitia Nairobi. Rais William Ruto wa Kenya na mwenzake wa Uganda,…
Serikali ya Tanzania yatakiwa kubuni sheria maalumu ya ukatili dhidi ya wanawake
Serikali ya Tanzania imetakiwa kubuni sheria maalumu ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake. Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wameitaka serikali ya nchi hiyo kubuni sheria maalumu kwa ajili ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutokana na kuwepo kwa ongezeko la kubwa la ukatili katika kipindi cha hivi karibuni hali…
Maandamano ya Wazayuni dhidi ya Baraza la Mawaziri la Netanyahu katika Siku ya Nakba
Moja ya matukio muhimu yaliyojiri katika Siku ya Nakba mwaka huu ni maandamano yaliyofanywa na Wazayuni wanaopinga vita dhidi ya Gaza. Wazayuni hao waliandamana mbele ya jengo la Wizara ya Vita ya Israel huko Tel Aviv. Jana tarehe 15 Mei ilisadifiana na kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 76 ya Nakba. Kila mwaka, tarehe 14 na 15…
Waziri Mkuu wa Niger: Amerika haina haki ya kututaka tukatishe uhusiano wetu na Iran na Urusi
Waziri Mkuu wa Niger alisema kuwa Marekani inahusika na kusambaratika kwa uhusiano kati ya Washington na Niamey, na akasema: “Washington haina haki ya kututaka kukata uhusiano na Iran na Russia.” Kwa mujibu wa ripoti hii, Ali Mohman Lamin Zain aliishutumu Marekani kwa kuruhusu magaidi kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Niger, na Washington haikuilinda nchi…
Tanzania, moja kati ya nguzo muhimu dhehebu la Shia Ithnashariya barani Afrika
Katika miongo 4 iliyopita, idadi ya Mashia nchini Tanzania imeongezeka, na Kituo cha Ahl al-Bayt ambayo ni moja kati ya madhehebu ya dini ya Kiislamu, kimepata nguvu nyingi. Asilimia kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam, mojawapo ya miji ya kihistoria na muhimu nchini Tanzania na Afrika Mashariki, ni Waislamu kutoka kwenye dhehebu hili la…
IDMC: Kuna ongezeko kubwa la ukimbizi wa ndani unaosababishwa na migogoro duniani
Ripoti mpya ya Kituo cha Ufuatiliaji wa Ukimbizi wa Ndani (IDMC) inaonyesha kuwa migogoro na ghasia duniani zimesababisha ongezeko lisilo na kifani la idadi ya wakimbizi wa ndani kufikia mwisho wa 2023. Gazeti la Guardian linalochapishwa London nchini Uingereza, limenukuu taarifa ya Kituo cha Ufuatiliaji wa Ukimbizi wa Ndani (IDMC) chenye uhusiano na Baraza la Wakimbizi…