Habari

Reuters: BRICS kujadili mpango mpya wa kimataifa wa mabadilishano ya fedha

Reuters: BRICS kujadili mpango mpya wa kimataifa wa mabadilishano ya fedha

Russia itawasilisha pendekezo lake la mfumo mpya wa fedha wa kimataifa kwa mataifa mengine wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya BRICS katika mkutano wa kilele wa kundi hilo utakaofanyika wiki ijayo nchini humo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Reuters likinukuu waraka uliosambazwa na Moscow kwa waandishi wa habari kabla…

Sisitizo la Joe Biden la kudumisha uwepo wa kijeshi wa Marekani Asia Magharibi

Sisitizo la Joe Biden la kudumisha uwepo wa kijeshi wa Marekani Asia Magharibi

White House ilitangaza siku ya Jumanne kwamba, Rais Joe Biden wa Marekani ameiandikia barua Congress ya nchi hiyo akiifahamisha kwamba vikosi vya Marekani vitaendelea kubakia katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) kwa kuhofia jibu la Iran kwa chokochoko za utawala wa Kizayuni. Akizungumzia jibu la makombora la Tehran kwa mashambulizi ya Israel, Rais…

UN: Watu bilioni 1 wanaishi katika umaskini wa kupindukia

UN: Watu bilioni 1 wanaishi katika umaskini wa kupindukia

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa, zaidi ya watu bilioni moja wanaishi katika umaskini mkubwa, na karibu nusu yao wapo katika nchi zinazokumbwa na migogoro. Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa jana Alkhamisi na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP): Nchi zilizosumbuliwa na vita zina viwango vya juu vya uchochole katika viashiria vyote vya…

Baraza la Seneti Kenya lamuondoa madarakani Naibu Rais Gachagua

Baraza la Seneti Kenya lamuondoa madarakani Naibu Rais Gachagua

Baraza la Seneti nchini Kenya limeidhinisha uamuzi wa kumuondoa madarakani Naibu Rais wa nchi hiyo Rigathi Gachagua. Jana Baraza la Seneti la Kenya lilipiga kura na kuidhinisha kuondolewa ofisini kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kutokana na mashtaka 5 kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake, katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa. Maseneta 54 kati ya 67 walipiga…

Hamas yathibitisha rasmi kuuawa kwa Yahya al-Sinwar

Hamas yathibitisha rasmi kuuawa kwa Yahya al-Sinwar

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilithibitisha rasmi kuuawa shahidi Yahya Sanwar, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati hio. “Khalil al-Hayya”, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, mchana wa leo (Ijumaa), katika ujumbe uliotangazwa kwenye mtandao wa “Al-Aqsa”, alithibitisha rasmi kuuawa shahidi “Yahya Al-Sinwar” , aliyekua mkuu…

Idadi ya waliokufa katika mlipuko wa lori la mafuta Nigeria yafikia 150

Idadi ya waliokufa katika mlipuko wa lori la mafuta Nigeria yafikia 150

Idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya lori la mafuta kuripuka na kusababisha moto mkubwa kaskazini magharibi mwa Nigeria imeongezeka na kufikia watu 150. Kwa muji wa msemaji wa jeshi la polisi, Lawan Adamu lori hilo liliripuka kando ya barabara kuu ya Kano-Hadejia kwenye eneo la Taura la jimbo la Jigawa la kaskazini magharibi mwa…

Israel inadai kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar ameuawa

Israel inadai kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar ameuawa

Israel inasema kua Sinwar aliuawa siku ya Jumatano kusini mwa Gaza. Israel inasema vikosi vyake vimemuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar huko Gaza. “Baada ya kukamilisha mchakato wa kutambua mwili, tumeweza kuthibitishwa kuwa Yahya Sinwar hayupo tena,” jeshi la Israeli lilisema. “Operesheni nyingi zilizofanywa na [jeshi la Israeli] na ISA [Shin Bet, ambayo ni huduma ya…

Tanzania yatakiwa kuheshimu haki za binadamu kuelekea uchaguzi serikali za mitaa

Tanzania yatakiwa kuheshimu haki za binadamu kuelekea uchaguzi serikali za mitaa

Shirika la kimatatifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Tanzania kulinda haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa. Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa serikali za mtaa tarehe 27 Novemba  mwaka huu huku wapiga kura wakitarajiwa kuchagua Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la…