Msafara wa baharini wa Lebanon waelekea mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kulinda maliasili zake
Msafara wa majini wa Lebanon umeanza safari yake ya kuelekea mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa lengo la kulinda utajiri wa nchi hiyo wa maliasili za mafuta na gesi dhidi ya uporaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, msafara wa majini wa Lebanon ambao uliandaliwa…
Mkuu wa zamani wa jeshi la Kizayuni: Israel haiwezi kuishambulia kijeshi Iran
Mkuu wa zamani wa majeshi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Shaul Mofaz amesema, Wairani ni watu werevu sana na wanao uwezo wa kuhakikisha wanapata haki zao za kinyukilia; na akakiri kwa kusema, Tel Aviv haina uwezo wa kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Tehran. Mofaz ameyasema hayo katika mahojiano na Kanali 12 ya…
Nigeria yaomba kuwa na ushirikiano wa kijeshi na Iran
Mwanadiplomasia mstaafu na mzoefu wa Nigeria Babaji Umar Misau amesema, ana matumaini kuwa nchi yake itaendelea kuwa na ushirikiano mzuri na wenye manufaa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo rafiki yake wa zamani kama ilivyokuwa kwa miongo mingi. Misau ambaye ni balozi wa zamani wa Nigeria katika nchi za Burkina Faso, Kenya na Somalia, amezungumzia umuhimu…
Taliban: Hatuna mpango wa kuutambua rasmi utawala haramu wa Israel
Msemaji wa Ofisi ya Kisiasa ya Taliban nchini Qatar amesema kuwa, kundi hilo halina mpango wa kuutambua rasmi utawala haramuu wa Israel. Mulla Muhammad Naeem amekanusha taarifa za baadhi ya vyombo vya habari vinavyoeleza kwamba, kundi la Taliban halina tatizo na nchi yoyote ile ukiwemo utawala ghasibu wa Israel na kubainisha kwamba, amenukuliwa vibaya kwani huo…
Kiongozi Muadhamu: Jamhuri ya Kiislamu ilirejesha nyuma majoka yenye vichwa saba ya Uistikbari
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ikipata ilhamu ya Ahlu-Beiti (as) iliyashinda na kuyarejesha nyuma majoka yenye vichwa saba ya Uistikbari na ikasonga mbele kimaendeleo. Ayatullah Sayyiid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo leo alipoonana na wajumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Beiti (as)…
Umoja wa Mataifa unasaidia mamilioni ya waathirika wa mafuriko Pakistan
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba, yanawasaidia zaidi ya watu milioni 33 walioathirika na mafuriko nchini Pakistan baada ya mvua kunyesha kwa kiwango kikubwa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1200. Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umeeleza kusikitishwa na mafuriko ya Pakistan yaliyosababisha vifo zaidi ya 1200…
Israel imewaua Wapalestina zaidi ya 110 Mwaka huu
Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limeua Wapalestina zaidi ya 110 na kuwajeruhi wengine wengi hadi sasa mwaka huu. Katika taarifa, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Palestina, limesema “Hadi sasa mwaka huu, mashambulizi ya Jeshi la Utawala wa Israel yamewaua Wapalestina 111, watoto 24 na wanawake 8.” Aidha taarifa hiyo imebaini kuwa,…
HAMAS: Vita dhidi ya Israel vitaendelea mpaka mateka wote wa Kipalestina watakapoachiliwa huru
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa, vita dhidi ya utawala haramu wa Israel vitaendelea mpaka pale mateka wote wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala huo ghasibu watakapoachiliwa huru. Hayo yameelezwa na Zaher Jabarin, afisa wa Hamas anayeshughulikia faili la mashahidi na mateka wa Palestina na kueleza kwamba, harakati hiyo haitapata utulivu na…