Nusu ya wananchi wa Saudia wanalalamikia ugumu wa maisha
Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, nusu ya wananchi wa Saudia Arabia wanalalamikia ugumu wa maisha na kupanda vibaya kwa bei za bidhaa. Kwa mujibu wa al Khalij al Jadid, uchunguzi huo wa maoni umefanywa na shirika moja la kibiashara la eneo hili baada ya kuombwa kufanya hivyo na taasisi ya Marekani…
Mshikamano kambi ya muqawama, ujumbe wa Hamas wakutana na Sayyid Nasrullah
Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon mjini Beirut, ukiwa ni ushahidi wa kuzidi kushikamana kambi ya muqawama katika eneo hili. Shirika la habari la Quds limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ujumbe huo wa ngazi za juu wa HAMAS…
Makamu wa Rais wa Iran: Marekani na Ulaya hazina njia nyingine ghairi ya kukubali JCPOA
Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na masuala ya uchumi amesema, vikwazo na mashinikizo ndiyo silaha ya mwisho kabisa ya Marekani na Ulaya na akaeleza kwamba katika hali ya sasa wao hawana njia nyingine isipokuwa kuyakubali mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Mohsen Rezaee aliyasema hayo hapo jana alipohutubia kabla ya Sala ya Ijumaa ya mjini…
Rais wa Syria asisitiza ulazima wa kupambana na misingi ya kifikra ya ugaidi
Rais Bashar al Assad wa Syria amesisitiza ulazima wa kupambana na misingi ya kifikra ya ugaidi na akaeleza kwamba, kupambana na ugaidi hakutawezekana kwa kutumia nguvu za kijeshi pekee, kwa sababu idiolojia ya mitazamo ya kufurutu ada haitambui mipaka bali inajipanua na kuenea kwa kasi kutoka nchi moja hadi nyingine. Rais wa Syria ameyasema hayo…
Mashambulizi haramu ya Marekani nchini Syria, nembo ya ubeberu wa Washington
John Kriby, mratibu wa mahusiano ya kiistratijia ya baraza la usalama wa taifa la ikulu ya Marekani, White House amejaribu kuhalalalisha mashambulio haramu ya nchi yake huko Syria na kudai kuwa, eti Washington haina nia ya kuzidisha machafuko katika eneo hili. Vile vile amedai kuwa, lengo la mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani huko Syria…
Palestina yataka uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa lakini Marekani inapinga
Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeanzisha tena msukumo wake wa kutaka uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa (UN) huku Marekani ikiendeleza njama zake za muda mrefu za kupinga hatua hiyo. “Tunajadiliana kwa nia njema na wanachama wote Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” amesema Riyad Mansour, balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa huku…
Watu 180 waaga dunia kutokana na mafuriko nchini Afghanistan
Watu wasiopungua 180 wamefariki dunia nchini Afghanistan kutokana na mafuriko na matukio yanayohusiana na mvua kali zilizonyesha hivi karibuni. Msemaji wa serikali ya Taliban nchini humo, Zabihullah Mujahid amesema mbali na watu 182 kuaga dunia kwenye janga hilo la kimaumbile, wengine zaidi ya 250 wamejeruhiwa. Amesema nyumba zaidi ya 3,000 zimesombwa na maji ya mafuriko hayo na…
HAMAS: Jinai za Wazayuni haziwezi kusimamisha muqawama katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza kuwa, kujeruhiwa askari wa utawala dhalimu wa Israel katika mapigano katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni ishara ya wazi ya sisitizo la vijana wa Kipalestina juu ya kupambana na uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel Hazim Qassim amebainisha kuwa, vita na utawala…