Mashariki ya kati

Jeshi la Syria lauzuia msafara wa magari sita ya kijeshi wa askari wa Marekani

Jeshi la Syria lauzuia msafara wa magari sita ya kijeshi wa askari wa Marekani

Vikosi vya jeshi la Syria vimeuzuia msafara wa askari wa jeshi la Marekani kuvuka eneo la kaskazini mashariki ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria SANA, msafara huo uliojumuisha magari sita ya kijeshi ya askari vamizi wa Marekani yakiandamana na gari moja la wanamgambo wa Kikurdi wa Syria wa kundi la…

Wanajeshi wa Israel waendeleza jinai katika maeneo tofauti ya Palestina

Wanajeshi wa Israel waendeleza jinai katika maeneo tofauti ya Palestina

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanaendelea na jinai zao dhidi ya Wapaelstina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kanali ya Telegram ya al Risala imesambaza mkanda wa video leo Jumanne unaoonesha jinai za wanajeshi makatili wa Israel na jinsi wanavyovamia na kufanya ukatili dhidi ya Wapalestina katika mji wa al Khalil wa…

Kuendelea wizi na uharamia wa Marekani wa kuiba mafuta ya Syria

Kuendelea wizi na uharamia wa Marekani wa kuiba mafuta ya Syria

Wizi na usafirishaji kimagendo mafuta ya Syria ungali unaendelea kufanywa na wanajeshi wa Marekani na wanamgambo wenye mfungamano nao katika ardhi ya nchi hiyo. Tangu mwaka 2011, wakati Syria ilipolazimishwa kuingia kwenye vita vya kupambana na magaidi, mbali na Marekani kuyaunga mkono baadhi ya makundi ya magaidi hao imekuwa ikilipa kipaumbele pia suala la uporaji wa…

Hamas yaishukuru Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa Palestina

Hamas yaishukuru Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa Palestina

Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina. Mahmoud al-Zahar ameyasema hayo Jumatatu katika mahojiano na Radio ya Al Aqsa. Amesema Iran imekuwa ikiunga mkono harakati dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia kwa mabavu ardhi…

Zaidi ya nusu karne sasa tangu kufanyika jinai ya kuchomwa moto Msikiti wa al-Aqswa

Zaidi ya nusu karne sasa tangu kufanyika jinai ya kuchomwa moto Msikiti wa al-Aqswa

Jumapili ya jana tarehe 21 Agosti ilisadifiana na kutimia mwaka wa 53 tangu kuchomwa moto Msikiti mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Wiaslamu, jinai ambayo ilifanywa na utawala vamizi wa Israel ambapo walimwengu walibakia kuwa watazamaji tu na kutoonyesha radiamali yoyote kwa kitendo hicho cha kinyama. Tarehe 21 Agosti 1969 Mzayuni mmoja aliuchoma moto…

Wafungwa wa Palestina waanza mgomo wa kula

Wafungwa wa Palestina waanza mgomo wa kula

Mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel wameanzisha mgomo usio na kikomo wa kula chakula. Shirika la habari la Palestin al-Yaum limeinukuu Bodi ya Wafungwa Wapalestina ikisema kuwa, hali ya taharuki imetanda katika jela na magereza ya utawala wa Kizayuni, baada ya mateka hao wa Kipalestina kuanza mgomo…

HAMAS yalaani hatua ya Polisi ya Ujerumani ya kufuatilia kauli ya Abbas kuhusu Holocaust

HAMAS yalaani hatua ya Polisi ya Ujerumani ya kufuatilia kauli ya Abbas kuhusu Holocaust

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, imelaani hatua ya maafisa wa Polisi ya Ujerumani ya kuamua kuchunguza matamshi aliyotoa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kusisitiza kuwa hatua hiyo inadhihirisha kuwa si kweli kama Berlin haipendelei upande wowote. Hivi karibuni, wakati Mahmoud Abbas maarufu kwa lakabu ya Abu Mazin…

Siku ya Kimataifa ya Misikiti; Palestina iko mstari wa mbele kulinda Msikiti wa al Aqsa

Siku ya Kimataifa ya Misikiti; Palestina iko mstari wa mbele kulinda Msikiti wa al Aqsa

Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds huko Palestina amesema kuwa, Msikiti huo mtakatifu bado uko kwenye moto wa jinai za Wazayuni lakini wananchi wa Palestina wataendelea kuwa mstari wa mbele kuulinda. Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ya Palestina OIC imeitangaza tarehe 21 Agosti kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Misikiti…