Mashariki ya kati

Wazayuni wajuta kumshinikiza Trump ajitoe katika makubaliano ya nyuklia JCPOA mwaka 2018

Wazayuni wajuta kumshinikiza Trump ajitoe katika makubaliano ya nyuklia JCPOA mwaka 2018

Wakuu wa masuala ya usalama wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wameonyesha majuto kwa hatua ya utawala huo ya kumshinikiza rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ajitoe kwenye makubaliano ya nyuklia JCPOA mwaka 2018. Ripoti iliyotolewa na chaneli ya televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya KAN 11 kuhusu mazungumzo yanayohusiana na makubaliano ya…

Sheikh Ikrima Sabri: Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu

Sheikh Ikrima Sabri: Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu

Khatibu wa msikiti mtakatifu wa al-Aqswa huko Palestina amesema kuwa, Quds na Msikiti wa al-Aqswa vinapitia kipindi kigumu kabisa. Sheikh Ikrima Sabri amesema kuwa, moto katika Msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu bado haujazimika. Akizungumza kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka ambao Wazayuni walikichoma moto Kibla cha Kwanza cha Waislamu…

Ibrahim Raeisi: Hakuna mazungumzo yoyote yatakayoifanya Iran ilegeze msimamo katika haki zake

Ibrahim Raeisi: Hakuna mazungumzo yoyote yatakayoifanya Iran ilegeze msimamo katika haki zake

Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakuna kikao au mazungumzo yoyote yale ambayo yatalifanya taifa hili lilegeze kamba na kufumbia macho haki zake. Rais wa Iran amesema hayo leo katika mkutano wa 17 wa Siku ya Kimataifa ya Msikiti na kueleza kwamba, serikali inafanya kila iwezalo na kwa nguvu zake…

Russia: Tutazipiga na chini sarafu za dola na euro kwa kushirikiana na waitifaki wetu

Russia: Tutazipiga na chini sarafu za dola na euro kwa kushirikiana na waitifaki wetu

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, Moscow inaimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na nchi marafiki zake na kwamba ina uhakika kwa ushirikiano huo itaweza kuziangusha sarafu za dola na euro kwani sarafu hizo ni sumu. Kwa mujibu wa ripoti ya leo Jumamosi ya shirika la habari la IRNA, Alexander Pankin amesema hayo…

Salami: Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan umo mbioni kujizatiti kwa silaha dhidi ya Wazayuni

Salami: Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan umo mbioni kujizatiti kwa silaha dhidi ya Wazayuni

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel yamefika hadi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuongeza kuwa, hivi sasa eneo hilo limo mbioni kujizatiti kwa silaha kwa ajili ya kukabiliana na Wazayuni maghasibu. Brigedia Jenerali Hussein Salami sambamba…

Uhusiano wa Uturuki na Israel walipiga jambia kwa nyuma taifa la Palestina

Uhusiano wa Uturuki na Israel walipiga jambia kwa nyuma taifa la Palestina

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Ukombozi wa Wananchi wa Palestina amelaani vikali hatua ya Uturuki ya kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. Jumatano iliyopita, Uturuki na utawala wa Kizayuni zilikubaliana kufufua uhusiano baina yao baada ya kusimama kwa muda wa miaka minne. Mwaka 2018 Uturuki ilisimamisha uhusiano…

Yemen yaonya kuhusu harakati za kutia shaka za askari wa US, Ufaransa

Yemen yaonya kuhusu harakati za kutia shaka za askari wa US, Ufaransa

Bunge la Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen limetadharisha kuhusu harakati na nyendo za kutiliwa shaka za wanajeshi wa Marekani na Ufaransa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu. Katika taarifa, Bodi ya Uongozi ya Bunge la Yemen imesema harakati hizo za wanajeshi wa Marekani na Ufaransa ambao ni waungaji…

Oman yasisitizia msimamo wake wa kutoruhusu ndege za Israel kutumia anga yake

Oman yasisitizia msimamo wake wa kutoruhusu ndege za Israel kutumia anga yake

Oman imesisitizia msimamo wake wa kukataa kuruhusu ndege za utawala wa haramu wa Israel kuruka katika anga yake. Wakati Oman ikiendelea kusisitizia msimamo wake huo, gazeti moja ya Kiebrania limedai kwamba, eti mashinikizo ya Iran ndiyo yanayoufanya utawala wa Oman kung’ang’ania msimamo huo. Gazeti la Israel Hayom lilidai katika chapisho lake jana kwamba, msimamo huo…