Mashariki ya kati

Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku

Marekani inaiba 80% ya mafuta yanayozalishwa Syria kila siku

Marekani inapora asilimia 80 ya mafuta yanayozalishwa kwa siku nchini Syria. Wizara ya Mafuta ya Syria imesema vikosi vamizi vya Marekani vinaiba mapipa 66,000 za mafuta ghafi kwa siku katika nchi hiyo ya Kiarabu. Kwa mujibu wa wizara hiyo, kiwango hicho kinachoibiwa na wanajeshi vamizi wa Marekani katika nch hiyo inayoshuhudia vita tangu mwaka 2011,…

HAMAS: Muqawama ndio njia bora kabisa ya kuikomboa ardhi ya Palestina

HAMAS: Muqawama ndio njia bora kabisa ya kuikomboa ardhi ya Palestina

Mjumbe mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, muqawama na mapambano ndio njia bora kabisa ya kuzikomboa ardhi za Palestina na kuifanya Palestina kuwa huru. Ismail Ridhwan amesisitiza kuwa, jibu la Wapalestina kwa jinai za utawala ghasibu wa Israel unaokalia Quds kwa mabavu litakuwa ni mtutu wa bunduki. Kiongozi huyo…

Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza

Israel yakiri kuwaua watoto Wapalestina Gaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwaua watoto watano Wapalestina katika hujuma yake ya hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Utawala huo dhalimu ulianzisha  vita dhidi ya Gaza mnamo Agosti 5 na vita hivyo vilimalizika baada ya siku tatu kufuatia upatanishi wa Misri. Jumla ya watu 49 waliuawa shahidi katika hujuma hiyo ya Israel…

Saudia yamhukumu mwanaharakati wa kike kifungo cha miaka 34 jela

Saudia yamhukumu mwanaharakati wa kike kifungo cha miaka 34 jela

Kundi la Freedom Action lilitangaza kuwa mahakama ya Al Saud ilimhukumu mwanaharakati wa haki za binadamu Salmi al-Shahab kifungo cha miaka 34 jela. Kwa mujibu wa kundi hilo lenye makao yake makuu mjini Washington, al-Shahab, mama wa watoto wawili, alikuwa akiishi Uingereza na alikamatwa akiwa safarini kuelekea nchini mwake. Akiwa Mshia, kila mara alitweet kuhusu…

Kukiri Mkuu wa Sera za Nje wa EU kwamba Magharibi imeonyesha undumakuwili katika kadhia za Ukraine na Gaza

Kukiri Mkuu wa Sera za Nje wa EU kwamba Magharibi imeonyesha undumakuwili katika kadhia za Ukraine na Gaza

Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amekiri kuwa nchi za Magharibi zinatumia vipimo vya nyuso mbili na za undumilakuwili kuhusiana na masuala ya kimataifa. Akijibu suali aliloulizwa katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa, kuhusu msimamo wa Umoja wa Ulaya kwa watu wa Ukraine na Gaza; pamoja na Borrell kukiri kuwa vimetumika vipimo vya…

DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi

DAESH (ISIS) wametumia asilimia 90 ya silaha za Marekani katika operesheni za kigaidi

Mtaalamu mmoja wa masuala ya kiusalama amesema, asilimia 90 ya wahanga na waathirika wa ugaidi nchini Iraq hasa katika maeneo yaliyokombolewa wameuliwa kwa silaha za Marekani. Japokuwa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh limeshindwa na kusambaratishwa katika nchi za Iraq na Syria, mabaki ya magaidi wa kundi hilo yangaliko katika nchi hizo na Marekani…

Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi

Iran: Muqawama wa Kiislamu hauishii tu katika ukanda wa Asia Magharibi

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muqawama na mapambano ya Kiislamu si kitu cha kuishia kwenye eneo moja tu. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA,  Ali Bahadori Jahromi alisema hayo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa mnasaba wa tarehe 23 Mordad kwa kalenda ya Kiirani ya…

Kani: Israel inakoseshwa usingizi na kizazi kipya cha Wapalestina

Kani: Israel inakoseshwa usingizi na kizazi kipya cha Wapalestina

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema kuwaua watoto wa Kipalestina kumegeuka na kuwa jambo la kawaida kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, na umwagaji damu huo unadhihirisha wazi kuwa Wazayuni wanakiogopa kizazi kipya cha Wapalestina. Ali Bagheri Kani alisema hayo jana hapa Tehran katika mazungumzo yake na Mohammed bin Abdulaziz al-Khulaifi,…