
HRW: Maadamu Israel haiadhibiwi, mashambulio dhidi ya Gaza yataendelea
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema, kutoadhibiwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndiko kunakoufanya utawala huo uendeleze hatua unazochukua. Katika taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Human Rights Watch imesema, Wapalestina zaidi ya 40, wakiwemo watoto 15 wameuawa katika vita vya siku tatu za karibuni kati ya utawala…

Wairani waandamana kulaani ukatili wa Israel dhidi ya wakazi wa Gaza
Wananchi wa Iran jana Jumanne walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani jinai za utawala wa Kizayuni za kuwaua shahidi wanawake na watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza. Maelfu ya waandamanaji walioshiriki kwenye maandamano hayo walikusanyika katika Medani ya Palestina jijini Tehran, karibu na ubalozi wa Palestina nchini Iran huku wakiwa wamebeba bendera za…

Raia Wapalestina 45 wameuawa shahidi katika siku 3 za hujuma za kikatili za Israeli huko Gaza
Siku tatu za mashambulizi ya utawala haramu wa Israel huko Gaza yamesababisha vifo vya raia Wapalestina 45 wakiwemo watoto 15 na wanawake wanne huku wengine 360 wakijeruhiwa Hayo yameripotiwa baada ya mapatano ya usitishaji vita kutangazwa kuanzia saa tano usiku jana Jumapili kwa saa za Gaza (20:30 GMT). Tangu Ijumaa, utawala wa Kizayuni wa Israel…

Nasrullah: Makombora ya muqawama yameilazimisha Israel isalimu amri
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema maadui Wazayuni wametangaza kuwa wako tayari kufikia makubaliano ya usitishaji vita baada ya makombora na maroketi ya wanamuqawama wa Ukanda wa Gaza kuutiwa kiwewe na wahakama utawala huo wa Kizayuni. Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo jana Jumapili na kuongeza kuwa, “Napongeza uthubutu wa Palestina kujibu mapigo, kwa…

Kiongozi Muadhamu ashiriki katika maombolezo ya Tasua ya Imam Husain AS
Usiku wa kuamkia leo umesadifiana na usiku wa mwezi tisa Mfunguo Nne, Muharram, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Tasua ya Imam Husain AS. Maombolezo ya usiku wa kuamkia leo yamefanyika katika kona zote za Iran na nje ya Iran ikiwemo Husainia ya Imam Khomeini MA mjini Tehran na kuhudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa…

HAMAS: Jihadi na mapambano yataendelea hadi kitakapokombelewa Kibla cha Kwanza cha Waislamu
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa tamko rasmi na sambamba na mkono wake wa pole kufuatia kuuwa shahidi Khalid Mansour, mmoja wa makamanda wa Brigedi za Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad al Islami ya Palestina, imesema kuwa, mapambano yataendelea hadi utakapokombolewa Msikiti wa al Aqsa ambao ndicho Kibla cha…

Watoto 6 ni katika Wapalestina 24 waliouliwa kikatili na Wazayuni tangu Ijumaa
Idadi ya Wapalestina waliouliwa shahidi katika jinai zinazoendelea za utawala wa Kizayuni huko Ghaza imeongezeka na kufikia watu 24 wakiwemo watoto wadogo sita. Utawala katili wa Israel unaoua watoto wadogo bila kiwewe, ulianzisha mashambulizi makubwa juzi Ijumaa dhidi ya maeneo ya makazi ya watu huko Ghaza na hadi leo Jumapili, mashambulio hayo yanaendelea. Wizara ya…

Jinai ya utawala wa Kizayuni katika kuishambulia Jihad Islami ya Palestina
Ijumaa alasiri, jeshil la utawala wa kigaidi wa Israel lilitekeleza jinai kubwa dhidi ya Wapalestina kupitia mashambulizi yaliyopewa jina la “Operesheni ya Alfajiri”, katika maeneo yanayodhibitiwa na harakati ya Palestina ya Jihad Islami katika Ukanda wa Gaza. Katika jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni, Wapalestina 12 akiwemo mtoto wa miaka 5, pamoja na Taysir al-Jabari,…