
Raisi: Kuuawa shahidi kidhulma Imam Hussein (AS) kunathibitisha umuhimu mkubwa wa kuamrisha mema na kukataza maovu katika dini ya Uislamu
Rais Ebrahim Raisi amesema, kuuawa shahidi kidhulma Imam Hussein (AS) ni ithibati kwamba kuamrisha mema na kukataza maovu kuna umuhimu mkubwa katika dini ya Uislamu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo katika mkutano na wajumbe wa tume ya kuhuisha uamrishaji mema na ukatazaji mabaya. Katika mkutano huo na wajumbe hao, Seyyid Ebrahim…

Mapigano yazuka baina ya askari wa mpakani wa Iran na wapiganaji wa Taliban
Gavana wa mji wa Hirmand ulioko kaskazini ya mkoa wa Sistan na Baluchistan kusini mashariki mwa Iran amesema, yamezuka mapigano kati ya askari wa kikosi cha mpakani cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wapiganaji wa kundi la Taliban la Afghanistan. Meysam Barazandeh, Gavana wa mji wa Hirmand ulioko mkoani Sistan na Baluchistan ameliambia shirika la habari…

Makumi ya viongozi wa serikali ya Saudia watiwa mbaroni kwa kula rushwa
Serikali ya Saudi Arabia imewatia mbaroni maafisa 78 wa serikali kwa tuhuma za ufisadi, kula rushwa, utapeli, kutakatisha fedha na kutumia vibaya madaraka yao. Taasisi ya kupambana na ufisadi nchini Saudi Arabia, kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikichunguza kesi nyingi za ubadhirifu na ufisaidi na hadi hivi sasa mamia ya wafanyakazi wa hivi sasa na…

Sheikh Naim Qassem: Israel haina budi kutambua rasmi haki za maliasili za Lebanon
Naibu Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna budi kuzitambua rasmi haki za Lebanon zinazohusiana na utajiri wa maliasili za baharini. Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo katika majlisi kuu ya Ashura na kusisitiza kuwa, Wamarekani inawapasa waache kushirikiana na Wazayuni katika kutafuta na kuchimba gesi katika eneo la…

Tawi la kijeshi la HAMAS lawaonyesha askari wawili wa Israel linaowashikilia mateka
Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS zimetoa taswira, sambamba na kuwahutubu Wazayuni kwamba: viongozi wa utawala wa Kizayuni wanakuambieni uongo kuhusu mateka. Julai 2014, Brigedi za Izzuddinl-Qassam zilitangaza kuwa zimemkamata mateka Shaul Aron askari wa Kizayuni katika vita vya siku 51; na utawala wa Kizayuni ukatangaza…

Iran: Mpango wa kijeshi wa nyuklia wa Israel ni tishio kwa usalama wa dunia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema ustawi wa mpango wa kijeshi wa nyuklia wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuendelea kukataa utawala huo vituo vyake vya nyuklia vikaguliwe na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ni tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa. Nasser Kan’ani Chafi, Msemaji wa Wizara…

New York Times: Iran imekuwa msafirishaji nje mkubwa wa drone duniani
Gazeti la The New York Times la Marekani limewanukuu wataalamu mbalimbali wakisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa msafirishaji nje mkubwa wa ndege zisizo na rubani (drone) duniani na inazidi kueneza ushawishi wake katika maeneo tofauti ya hata nje ya Asia Magharibi. Shirika la habari la FARS limelinukuu gazeti hilo la Marekani likidai kuwa,…

Iran inaunga mkono kikamilifu sera ya ‘China Moja’, inapinga ‘uharibifu’ wa Marekani
Rais wa Iran Ebrahim Raisi anasema kuheshimiwa mamlaka ya kitaifa na kulindwa mipaka ya ardhi ya nchi ni miongoni mwa kanuni za kimsingi za sera za kigeni za Tehran huku akitangaza uungaji mkono thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu kwa sera ya China Moja kuhusiana na Taiwan. “Uungaji mkono kwa sera ya China Moja ni sera…