
Nasrallah: Hizbullah ilikataa hongo ya Marekani kusitisha makabiliano na Israel
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema harakati hiyo ilikataa mapendekezo kadhaa ya hongo ya kifedha ya Marekani ili kusitisha mapambano yake na utawala wa Kizayuni wa Israel . Katika mahojiano ya aina yake yaliyorekodiwa miaka 20 iliyopita na kurushwa hewani wiki hii, Katibu Mkuu wa Hezbollah Sayyed Nasrallah anasema harakati hiyo ya mapambano…

Mfalme wa Bahrain amuuzulu waziri wake kwa kukataa kumpa mkono balozi wa Israel
Mfalme wa Bahrain amemuuzulu waziri mwanamke wa nchi hiyo kwa kukataa kumpa mkono balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa mjini Manama na kwa kupinga hatua ya kuanzisha ya uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu. Tovuti ya habari ya Shahab News imeripoti kuwa, hivi karibuni ilifanyika hafla katika makazi ya balozi wa Marekani…

Iran yavunja mtandao wa majasusi wa Mossad ya Israel
Wizara ya Intelijensia ya Iran imetangaza habari ya kutiwa mbaroni majasusi kadhaa waliokuwa wakitumikia shirika la ujasusi la Israel (Mossad). Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa, vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu vimewatia nguvuni majasusi hao waliojipenyeza nchini kupitia eneo la Kurdistan, magharibi mwa Iran. Kwa mujibu wa Wizara ya Intelijensia ya Iran, maajenti hao…

Joseph Mbilinyi (Sugu): Kuna maana gani Tanzania kufungua ubalozi wake Israel na kuwaacha Wapalestina
Mbunge wa Mbeya mjini wa chama cha upinzani nchini Tanzania (CHADEMA) Joseph Osmund Mbilinyi maarifa kwa jina la Sugu amesema kuwa, inashangaza kuona hii leo serikali ya Rais John Magufuli inakwenda kinyume na misingi iliyojengwa na Tanzania katika kuwatetea watu wanaokandamizwa duniani, hususan Palestina. Akitoa mfano wa suala hilo mheshimiwa Mbilinyi ameelezea namna ambavyo Tanzania…

Jeshi la Syria latungua makombora ya Israel viungani mwa Damascus
Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Syria kimetangaza kutungua makombora yaliyokuwa yamevurumishwa na utawala haramu wa Israel nje ya mji mkuu Damascus. Shirika rasmi la habari la Syria, SANA limetangaza kuwa, mizinga ya ulinzi wa anga ya Syria alfajiri ya leo Ijumaa imetungua akthari ya makombora hayo ya Israel viungani mwa Damascus. Jeshi katili…

Wabunge Ufaransa walaani sera za apathaidi za Israel
dadi kubwa ya wabunge katika Bunge la Kitaifa la Ufaransa wametia saini rasimu ya azimio la kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na sera zake za ubaguzi wa rangi au apatahidi na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina. Azimio hilo ambalo lina kichwa kisemacho: “Kutaasisishwa Utawa wa Apathaidi Dhidi ya Watu wa Palestina” limeidhinishwa…

Tanzania kuitumia Israel kutatua mgogoro wa Palestina
Haya yalikuwa ni maoni na mawazo ya mmoja wa Wanasiasa wa Tanzania kuhusu Palestina na Israel. Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro amesema Tanzania haitaitenga Israel katika mchakato wa kusaka amani katika mgogoro wake na Palestina. Hivi karibuni Balozi wa Palestina nchini Tanzania,…

Kukiri wataalamu wa Kizayuni kuwa uwezo wa nyuklia wa Iran hauwezi kuharibiwa kijeshi
Katika kujibu maneno ya Dakta Kamal Kharrazi Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Sera za Kigeni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mkuu wa Majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel amezungumzia kile amekitaja kuwa tishio la Iran na chaguo la kijeshi na kusema chaguo…