
Iran: Israel ndio mzizi wa ugaidi na ukosefu wa usalama Asia Magharibi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio chimbuko la vitendo vya kigaidi na ukosefu wa usalama na uthabiti katika eneo hili la Asia Magharibi. Naser Kan’ani alisema hayo jana Jumanne na kuongeza kuwa, hatua ya Marekani kuukingia kifua na kuunga mkono utawala…

Maseneta waitaka serikali ya Biden kuwajibika kuhusu uchunguzi wa mauaji ya Shireen
Maseneta wa chama cha Democratic cha Marekani wameitaka serikali ya Rais Joe Biden wa nchi hiyo kuwajibika kuhusu uchunguzi unaohusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Palestina wa televisheni ya Al Jazeera, Shireen Abu Akleh. Ni baada ya Umoja wa Mataifa kumesema kuwa taarifa ulizokusanya zinaonesha kuwa, Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa televisheni ya…

MAREKANI, TANZANIA KIWAKILISHI CHA ‘DUNIA’ MBILI KATI YA TATU ZINAZOKIDHANA KUHUSU ISRAEL
Uchambuzi wa Kisiasa kuhusu Uhusiano wa Tanzania na Israel. MAPEMA wiki iliyopita na wiki hii dunia imeshuhudia historia ikiwekwa kwa husiano za kidiplomasia linapokuja Taifa la Israel baada ya Tanzania na Marekani kwa nyakati hizo mbili tofauti kufungua balozi mpya katika Taifa hilo la Mashariki ya Kati. Wakati Tanzania ikifungua ubalozi mara ya kwanza nchini…

Hamas: Kuchomwa wakiwa hai wanajeshi wa Misri na utawala wa Israel kunadhihirisha dhati ya ukatili
Ikitoa radiamali yake kwa habari kuhusu kuchomwa wakiwa hai makumi ya wanajeshi wa Misri katika vita vya mwaka 1967; Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) imesema kitendo hicho kinadhihirisha dhati ya ukatili na kutenda jinai ya utawala wa Kizayuni. Gazeti la Yediot Aharanoth wiki hii lilifichua kuwa, utawala wa Kizayuni baada ya kupita zaidi ya miaka…

Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania walaani mauaji ya mwandishi wa Al-Jazeera
Dar es Salaam. Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania unalaani vikali mauaji ya kikatili ya Israel yaliyomlenga mwandishi wa habari mkongwe wa Al-Jazeera, Shireen AbuAqla katika kambi ya wakimbizi ya Jenin. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ubalozi huo Mei 11, 2022, wanajeshi wa Israel walimpiga risasi Shireen kichwani. Mwandishi huyo aliuawa wakati akiripoti uhalifu wa…

Tanzania inaathirikaje Jerusalem ukiwa mji mkuu Israel
Huu ni uchambuzi uliotolewa na mchambuzi wa Gazeti Mwananchi kuhusu kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem akisema: Hivi karibuni Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kwamba ubalozi wake utahamishwa kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem. Akitetea uamuzi huo, Trump alisema ulishapitishwa na Baraza la Congress…

Kiongozi wa Ansarullah: Saudia inawazuia baadhi ya Waislamu kutekeleza Hija kwa sababu za kisiasa
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, utawala wa Saudi Arabia unawazuia baadhi ya Waislamu kutekeleza ibada ya Hija kwa sababu ya misimamo ya kisiasa ya ukoo wa Aal Saud au misimamo ya Marekani na Israel dhidi ya Waislamu hao. Sayyid Abdul Malik Badruddin al-Houthi ametoa pongezi kwa Umma wa Kiislamu, mahujaji wa Nyumba ya…

Uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Palestina
Nyerere alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa Kiafrika kulitambua Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) chini ya Yasser Arafat na, mwaka 1973, Dar es Salaam ikawa makao ya ubalozi wa kwanza wa PLO barani Afrika. “Kizazi chetu kilikuwa kizazi cha mapambano ya utaifa kwa ajili ya uhuru wa nchi zetu … lakini hali ya…