
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Asia Magharibi haidhibitiwi tena na Marekani
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema eneo la Asia Magharibi halidhibitiwi tena Marekani, na kwamba hivi sasa lipo katika mikono ya mataifa ya Waislamu. Hujjatul-Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi-Fard amesema hayo katika hotuba za Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa Tehran na kuongeza kuwa, “Miito ya baadhi ya watu ya kutaka kuundwa muungano wa…

Shukrani za makundi ya muqawama, vyama vya Lebanon na Palestina kwa Iran.
Wawakilishi wa ngazi ya juu wa makundi ya mapambano, vyama vya kisiasa vya Lebanon na harakati za mapambano ya ukombozi za Palestina zimeshukuru na kupongeza misaada na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Makundi hayo yametoa pongeza na shukrani hizo katika hafla ya kumalizika muda wa kuhudumu balozi wa Iran mjini Beirut. Muhammad…

Rais wa Iran na Mfalme wa Qatar wabadilishana mawazo kuhusu mazungumzo ya uondoaji vikwazo.
Rais Ebrahim Raisi amesisitiza kuhusu misimamo ya wazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo vya kidhalimu lilivyowekewa taifa hili. Seyyid Ebrahim Raisi ametoa sisitizo hilo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani. Katika mazungumzo hayo, Rais Raisi ameashiria ripoti kadhaa…

China yaitaka Marekani kurekebisha makosa yake mkabala wa Iran
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya China imesema kuwa Washington, ikiwa ni mwanzilishi wa mgogoro wa nyuklia wa Iran, inapaswa kurekebisha makosa yake na kujibu wasiwasi wa Tehran. Beijing imekuwa ikiilaumu Marekani mara kwa mara kwa hali ya sasa ya miradi ya kuzalisha nishati ya…

Borrell: Lengo la mazungumzo ya Doha ni kuhuisha utekelezaji wa mapatano ya JCPOA
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya (EU) ameandika katika ujumbe wake wa twiter kwamba lengo la mazungumzo ya Doha ni kuanza kufanya kazi mapatano ya JCPOA. Baada ya mazungumzo ya Vienna kusita kwa miezi kadhaa; mazungumzo hayo kwa mara nyingine tena yalianza jana Jumanne huko Doha mji mkuu wa Qatar kwa kuhudhuriwa…

Raisi: Uwepo wa utawala wa Kizayuni unadhoofisha usalama wa eneo
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel unaibua taharuki na kudhoofisha usalama wa eneo hili la Asia Magharibi. Rais wa Iran, Sayyid Ebrahim Raisi alisema hayo jana Jumatano katika kikao na mwenzake wa Azerbaijan, Ilham Aliyev, pambizoni mwa Mkutano wa 6 wa Nchi Zinazopakana na Bahari ya Kaspi huko Ashgabat,…

Raisi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaitambua Bahari ya Kaspi kuwa bahari ya amani na urafiki
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika Mkutano wa Sita wa Nchi za Pwani mwa Bahari ya Kaspi kuwa: Iran inaitambua bahari hiyo kuwa ni bahari ya amani na urafiki na kiunganishi cha watu wa eneo hili. Sayyid Ebrahim Raisi amesisitiza kuwa Iran iko tayari kwa ajili ya ushirikiano wa pande zote kwa…

Marais wa Iran na Russia wanakutana leo Ashgabat
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo anakutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin katika kikao kitakachofanyika katika mji mkuu wa Turkmenistan, Ashgabat. Kwa mujibu wa taarifa mshauri wa rais wa Russia katika sera za kigeni Yuri Viktorovich Ushakov amesema Rais Putin leo atashiriki katika kikao cha viongozi wa Nchi za Pwani ya…