Maandamano ya maelfu ya Wazayuni yanaendelea katika ardhi za Palestina
Maelfu ya Wazayuni wameendelea na maandamano yao ya kumpinga waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, katika miji ya Quds na Tel Aviv licha ya kuweko sherehe za miaka 75 ya kuasisiwa utawala haramu na pandikizi wa Israel. Tangu miezi minne nyuma, Wazayuni wanafanya maandamano kila wiki kupinga marekebisho ya serikali ya Benjamin Netanyahu…
Wanamambano kutoka Gaza walifanyia majaribio kombora la kutoka ardhini hadi angani
Vyanzo vya habari viliripoti majaribio ya kombora la kutoka ardhini hadi angani huko Gaza na vikosi vya upinzani. Vyanzo vya ndani vya Gaza vimeripoti leo (Alhamisi) jaribio la kombora la kutoka ardhini hadi angani katika anga ya eneo hili. Kwa mujibu wa Shahab News, kombora hili lilirushwa kuelekea baharini na baada ya hapo, sauti ya…
Amir-Abdollahian: Oman ina ubunifu mzuri kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, serikali ya Oman ina ubumifu mzuri kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran, ubunifu ambao utasaidia kurejea mazungumzo katika suala hilo. Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo akiwa ziarani nchini Oman jana Jumanne ambapo alipokewa na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Oman na…
Shambulio la silaha dhidi ya ofisi ya chama cha Erdogan mjini Istanbul
Vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti kwamba watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walishambulia moja ya ofisi za uchaguzi za chama tawala cha Haki na Maendeleo mjini Istanbul. Gazeti la “Daily Sabah” liliripoti Jumamosi kwamba ofisi ya uchaguzi ya Chama tawala cha Haki na Maendeleo cha Uturuki mjini Istanbul ililengwa na kundi la watu wasiojulikana wenye…
Sheikh Kazem Seddiqi: Marekani imeshindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ndani wa Israel
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, licha ya Marekani kuwa na mfungamano wote na utawala haramu wa Israel lakini imeshindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ndani wa utawala huo, na hilo ni ishara ya kutokuwa na uwezo. Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Kazem Seddiqi amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa…
Zaidi ya waumini 100,000 wahudhuria swala ya Eid al-Fitr katika Msikiti wa Al-Aqsa
Makundi tofauti ya wananchi wa Palestina wamefanya ibada ya Swala ya Eid al-Fitr katika maeneo tofauti ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu Ijumaa asubuhi ya leo. Takriban watu 120,000 waliswali swala ya Idi katika Msikiti wa Al-Aqsa. Licha ya utayarifu kamili wa jeshi la Kizayuni katika Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu na kuunda vizuizi vya kijeshi na…
Maelezo ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa wa Yemen kutoka kwa maneno ya mkuu wa kamati ya masuala ya wafungwa wa Yemen
Mkuu wa Kamati ya Wafungwa wa Serikali ya Kitaifa ya Wokovu ya Yemen amesisitiza kuwa Mabadilishano ya wafungwa wa Yemen ni oparesheni ya pili kwa ukubwa ni zoezi la kubadilishana wafungwa lililofanyika kupitia Umoja wa Mataifa na zoezi hili lilidumu kwa mda wa siku 3. Katika oparesheni hii, zaidi ya wafungwa 700 kutoka jeshi na…
Mapigano yameanza tena katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum
Ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kuwa mapigano yamezuka upya kati ya vikosi vya jeshi la Sudan vinavyoongozwa na Jenerali Abdel-Fattah al-Barhan na vikosi vya Radiamali ya Haraka RSF vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Daghlo maarufu kama Hamidati katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum. Chaneli ya televisheni ya Al-Jazeera imetangaza mapema leo kuwa mapigano kati ya…