Shambulio la uwanja wa ndege wa Aleppo; Mashambulizi kwenye njia kuu ya misaada ya kibinadamu
Habari : Utawala wa kibaguzi wa Kizayuni ulilenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aleppo kutoka upande wa Bahari ya Mediterania magharibi mwa Latakia kwa shambulio la kinyama la anga, shambulio lililosababisha uharibifu wa mali katika uwanja huo wa ndege na kuufanya kutotumika tena. Ni wazi kabisa kuwa uvamizi wa kibaguzi wa Israel ulianza kutoka…
Nyuma ya pazia na mienendo yenye kutia shaka ya Wamarekani katika majimbo inayokaliwa kwa mabavu ya Yemen
Sio siri kuwa Saudi Arabia imepata kipigo kikali baada ya kutumia makumi ya mabilioni ya dola katika vita visivyo na tija dhidi ya Yemen. Moja ya malengo ya Bin Salman kwa uchokozi wake huko Yemen ni kuwa karibu na duru za maamuzi za Marekani-Magharibi-Israel. Alitaka Salman aishambulie Yemen ili kukaribia zaidi matakwa ya duru hizi…
Nafasi ya wanawake wa Yemen katika kupinga muungano wa uchokozi
“Najiba Motahar”, mshauri wa ofisi ya rais wa Yemen katika masuala ya wanawake amesema kuwa wanawake wa Yemen wamekuwa na nafasi muhimu katika kukabiliana na vita vilivyowekwa dhidi ya taifa la Yemen kwa kuendelea na muqawama wao na kuwaunga mkono wanaume wanaopigana mbele. Mtandao wa Habari wa Al-Alam ulimkaribisha Bi. Najiba Motahar, mshauri wa ofisi…
Je, unatathimini vipi kurudi kwa Waarabu Syria?
Kurejea kwa Waarabu nchini Syria kupitia swala la kibinadamu baada ya zaidi ya muongo mmoja kumeibua hali kadhaa kuhusu mustakabali wa kisiasa wa nchi ya Syria. Waandishi na watafiti wa masuala ya kisiasa walisisitiza kuwa tetemeko la ardhi la Syria ni mwanzo wa kurejea kwa wakuu wa nchi za Kiarabu nchini Syria. Kama si upinzani…
Umoja wa Mataifa wapongeza msamaha wa Kiongozi Muadhamu kwa wafungwa waliokamatwa wakati wa ghasia
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Korosi amepongeza agizo la Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei la kutoa msamaha kwa idadi kubwa ya wafungwa wa Iran na kusema kuwa hatua hiyo inastahili kupongezwa. Korosi aliyasema hayo Jumanne alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian kando…
Wapalestina 3 walijeruhiwa katika mashambulizi ya wanajeshi wa Israel mjini Yeriko
Kufuatia mashambulizi ya wanajeshi hao wa Kizayuni katika kambi ya “Aqaba Jabr” katika mji wa Erija, ulioko kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, mapigano yalizuka kati ya wapiganaji hao wa Kipalestina na askari wa jeshi la Kizayuni. Duru za Palestina zimebainisha kuwa, wanajeshi hao wa Israel walishambulia kambi ya Aqaba Jabr na kuizingira…
Afisa wa kijeshi na mkuu wa operesheni ya ISIS, tawi la Khorasan auwawa mjini Kabul
Msemaji wa Taliban alitangaza kuwa Taliban Qari Fateh, ambaye ni afisa mkuu wa kijeshi na afisa wa operesheni wa tawi la Khorasan la ISIS aliuawawa mjini Kabul. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Jamuhuri, Jumanne hii msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid alitoa taarifa na kusema kuwa kutokana na oparesheni ya vikosi maalum…
Ansarullah: Njia ya amani nchini Yemen ni kuyafurusha majeshi ya kigeni
Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Ansarullah Yemen akizungumzia tukio la urushaji mawe mawe wa Marekani na Uingereza katika kadhia ya kibinadamu ya Yemen amesisitiza kuwa, njia ya amani inapitia lango la kadhia hii nayo ni kuyafukuza majeshi ya kigeni nchini humo. “Ali al-Qahoum” aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba kurushiwa mawe Marekani na…