Muungano unaolegalega wa utawala wa Kizayuni wakaribia kusambaratika
Duru za utawala wa Kizayuni wa Israel zimetangaza hbari ya kujiuzulu kiongozi mwingine wa serikali ya utawala huo bandia na hivyo kuongeza uwezekano wa kusambaratika muungano unaolegalega wa serikali yenye misimamo ya kufurutu ada ya Benjamin Netanyahu. Kwa siku kadhaa sasa utawala wa Kizayuni unashuhudia mapambano baina ya serikali mpya yenye misimamo mikali na wapinzani….
Hamas: Kutiwa nguvuni wanamuqawama kunakofanywa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kuihudumia Israel
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa radiamali kufuatia hatua ya idara za usalama za Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kuwatia nguvuni wanamuqawama na wanachama wa harakati hiyo katika Ukingo wa Magharibi na kusisitiza kuwa, kitendo hicho ni sawa na kuuhudumia utawala wa Kizayuni. Uratibu wa masuala ya usalama umeanzishwa kati ya…
Mkoloni kizee Mfaransa atimuliwa rasmi nchini Burkina Faso
Serikali ya Burkina Faso imeamua kusitisha mkataba wa kijeshi ulioruhusu wanajeshi wa Ufaransa wafanye wanalotaka nchini humo. Mkataba huo wa kijeshi ulikuwa umeipa nchi ya Ulaya ya Ufaransa haki kubwa kuliko hata raia wenyewe wa Burkina Faso. Ufaransa hivi sasa ina wanajeshi wake maalumu 400 katika nchi ya Afrika Magharibi. Serikali mpya ya Burkina Faso imesema,…
Kuanza tena uchunguzi kuhusu mlipuko wa bandari ya Beirut
Duru za habari za Lebanon zimetangaza kuwa hakimu anayechunguza kesi ya mlipuko uliotokea mwaka 2020 katika bandari ya Beirut ameamua kuanzisha tena uchunguzi wa kesi hiyo. Tareq Al-Bitar hakimu anayechunguza mlipuko katika bandari ya Beirut ameamua uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo uanzishwe tena. Baadhi ya duru za habari zimearifu kuwa, al Bitar ameamua kuwasilisha kesi mahakamani dhidi…
Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwauwa kwa makusudi raia wa Palestina
Jeshi la utawala wa Kizayuni limetoa taarifa na kukiri kwa namna isiyo rasmi kwamba lilimlenga na kumuua shahidi mwanamme wa Kipalestina bila ya sababu yoyote ile. Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa, shahidi Ahmad Hassan Kahlah ambaye wiki iliyopita aliuliwa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo huko Silwad katika mji wa…
Mtazamo mwingine kuhusu uwekezaji mkubwa wa Bin Salman katika michezo Saudia
Iwapo mtu yeyote atafuatilia habari za Saudi Arabia baada ya kunyakuliwa madaraka ya nchi hiyo ya kifalme na Mohammed bin Salman, atakumbana na mkanganyiko mkubwa katika mielekeo na sera za nchi hiyo. Moja ya matukio na mifano ya wazi katika uwanja huo ni kwamba, kwa upande mmoja, Bin Salman anataka kuonyesha sura inayoitwa ya kisasa…
Netanyahu azidi kupelekwa mchakamchaka, kiongozi mwingine wa serikali ajiuzuluu
Duru za utawala wa Kizayuni wa Israel zimetangaza hbari ya kujiuzulu kiongozi mwingine wa serikali ya utawala huo poandikizi na kuzidi kuipeleka mchakamchaka serikali yenye misimamo ya kufurutu ada ya Benjamin Netanyahu. Kwa siku kadhaa sasa utawala wa Kizayuni unashuhudia mapambano baina ya serikali mpya yenye misimamo mikali na wapinzani. Jumamosi wiki hii kulifanyika maandamano…
Uhusiano kati ya mumini na Imam ni uhusiano muhimu zaidi lakini uliotelekezwa – Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa shule Jamia Urwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa katika msikiti wa: Masjid Baitul ul Ateeq Lahore – Pakistan Januari 20, 2023 Hotuba ya 1: Rabetu – Uhusiano kati ya mumini na Imam ni uhusiano muhimu zaidi lakini uliotelekezwa Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu kumcha Mwenyezi Mungu,…