Mashariki ya kati

Mwanariadha  wa Yemen ajiondoa katika mashindano dhidi ya mwakilishi wa utawala wa Kizayuni

Mwanariadha wa Yemen ajiondoa katika mashindano dhidi ya mwakilishi wa utawala wa Kizayuni

Mwanariadha huyo wa Yemen alijiondoa katika mashindano hayo ili kuepusha makabiliano na mwakilishi wa utawala wa Kizayuni katika mashindano ya “Grand Prix” ya Ufaransa. Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Al-Ahed, “Ebrahim Al-Shabami”, mwanamieleka wa fremu wa kilo 66 wa Yemen, alitangaza kujiondoa baada ya kuchujwa dhidi ya mwanariadha kutoka utawala wa Kizayuni katika…

Maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen kulaani uhalifu wa kuchoma Qur’ani nchini Uswidi

Maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen kulaani uhalifu wa kuchoma Qur’ani nchini Uswidi

Wananchi wa Yemen walifanya maandamano makubwa katika uwanja wa Bab El-Iman huko Sana’a Jumatatu hii jioni kulaani uhalifu wa kuchoma Quran nchini Uswidi. Washiriki hao walionyesha hasira na kuchukizwa kwao kwa kuyatusi maeneo matukufu ya Kiislamu na kutaka kuchukua misimamo mikali ili kukomesha mashambulizi hayo ya mara kwa mara dhidi ya maeneo matukufu ya Kiislamu….

Bunduki 9,300 zimenaswa katika machafuko ya karibuni nchini Iran

Bunduki 9,300 zimenaswa katika machafuko ya karibuni nchini Iran

Msemaji wa Kamandi ya Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa silaha 9,300 zimekamatwa wakati wa machafuko yaliyozuka hapa nchini hivi karibuni. Kuanzia mwishoni mwa Septemba 2022, baadhi ya maeneo ya Iran yalikumbwa na machafuko; na katika siku zake za kwanza kabisa ilidhihirika wazi kuwa baadhi ya vyombo vya habari vina mkono katika kushamirisha…

Recep Tayyip Erdoğan: Uchaguzi wa rais Uturuki kufanyika Mei 14 mwaka huu

Recep Tayyip Erdoğan: Uchaguzi wa rais Uturuki kufanyika Mei 14 mwaka huu

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ametangaza kuwa, uchaguzi wa urais na wa Wabunge wa nchi hiyo utafanyika tarehe 14 Mei mwaka huu. Erdogan ametoa tangazo hilo jana kwa kusema: “Ninatumia mamlaka yangu kutangaza kuwa, uchaguzi wa rais na ule wa Bunge utafanyika tarehe 14 Mei mwaka huu. Akizungumza na vijana wanaotarajiwa kupiga kura kwa…

Kuendelea uingiliaji hasi wa Marekani katika masuala ya ndani ya Iraq

Kuendelea uingiliaji hasi wa Marekani katika masuala ya ndani ya Iraq

Marekani ingali inaendelea kuingilia masuala ya ndani ya Iraq kwa namna hasi, kwa kuzingatia nyenzo za mashinikizo ilizonazo mikononi mwake. Tangu mwaka 2003, Iraq imejionea enzi mpya katika siasa na muundo wake wa madaraka. Mnamo mwaka huo, Marekani iliishambulia na kuivamia kijeshi nchi hiyo na kuupindua utawala wa Kibaathi. Japokuwa tukio hilo lilihitimisha mfumo wa kidikteta…

Kukalia kuti kavu baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu

Kukalia kuti kavu baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu

Baraza la mawaziri la Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamiin Netanyahu halijafikisha hata muda wa mwezi mmoja ambapo tayari linakabiliwa na hatari ya kusambaratika. Serikali ya Netanyahu inakabiliwa na matatizo mawili makuu na ya kimsingi ambayo yameifanya ikabiliwe na hatari ya kusambaratika. Tatizo la kwanza ni maandamano makubwa na ya mapema ya wananchi…

Balozi mwingine wa Israel ajiuzulu kulalamikia serikali ya misimamo ya kufurutu mpaka ya Netanyahu

Balozi mwingine wa Israel ajiuzulu kulalamikia serikali ya misimamo ya kufurutu mpaka ya Netanyahu

Baada ya kujiuzulu balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Ufaransa, balozi wa utawala huo nchini Canada naye pia amejiuzulu wadhifa wake kulalamikia baraza la mawaziri lenye misimamo ya kufurutu ada linaloongozwa na Benjamin Netanyahu na kumuunga mkono waziri mkuu wa zamani Yair Lapid ambaye ni kiongozi wa wapinzani wa Netanyahu. Gazeti la kizayuni…

Mashambulio ya Saudia mpakani mwa Yemen yameua watu saba na kujeruhi 91

Mashambulio ya Saudia mpakani mwa Yemen yameua watu saba na kujeruhi 91

Duru za Yemen zimeripotiwa kuwa, tangu ulipoanza mwaka mpya wa 2023 hadi sasa, watu saba wameuawa na wengine 91 wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Saudi Arabia katika maeneo ya mpakani mwa Yemen. Kwa uungaji mkono wa Marekani, Muungano wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine kadhaa, Saudi Arabia iliivamia kijeshi Yemen mwezi Machi 2015…