Shahsia Muhimu

Mjukuu wa Mandela: Msimamo thabiti wa Wapalestina limekua ni jambo lenye kutuhamasisha

“Zuliville Mandela”, mjukuu wa “Nelson Mandela” na mjumbe wa Bunge la Afrika Kusini alisema: “Nia thabiti ya Wapalestina kupata uhuru wa nchi yao imekuwa msukumo katika kuibua suala la Palestina katika duru za kimataifa.” Zuliville Mandela ambaye alikwenda Istanbul kwa ajili ya kujadili na kuchunguza kadhia ya Palestina na uchokozi wa utawala ghasibu wa Kizayuni…

Sheikh Zakzaky: Nililia kwa furaha kwa sababu ya mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel

Sheikh Zakzaky: Nililia kwa furaha kwa sababu ya mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alitangaza kuwa, operesheni ya adhabu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni ilifufua matumaini katika nyoyo za watu wanaodhulumiwa na kukandamizwa duniani. Sheikh Ebrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiashiria operesheni ya adhabu ya Iran ya “Ahadi ya Kweli” dhidi ya utawala wa Kizayuni ametangaza…

‘Niko tayari kufa’: Hotuba ya Mandela iliyotikisa  mfumo ‘Apartheid’ (ubaguzi wa rangi)

‘Niko tayari kufa’: Hotuba ya Mandela iliyotikisa mfumo ‘Apartheid’ (ubaguzi wa rangi)

Miaka 60 iliyopita wakati wa Kesi ya Rivonia nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela alitoa hotuba moja maarufu katika karne ya 20. Alitarajia kuhukumiwa kifo lakini badala yake aliishi kuona ndoto yake ya ‘jamii ya kidemokrasia na huru’ ikitimia. “Mshtakiwa namba moja” alikuwa akizungumza kutoka kizimbani kwa karibu saa tatu wakati alipotamka maneno ambayo hatimaye yangeibadilisha…

Mkuu wa Majeshi na makamanda tisa waandamizi wa Kenya wafariki katika ajali ya helikopta

Mkuu wa Majeshi na makamanda tisa waandamizi wa Kenya wafariki katika ajali ya helikopta

Kenya inaomboleza kifo cha Mkuu wa Majeshi (KDF), Jenerali Francis Omondi Ogolla ambaye ameaga dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana Alkhamisi katika eneo la Sindar kwenye mpaka wa Kaunti ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet. Jenerali Ogolla alifariki dunia pamoja na maafisa wengine tisa waandamizi wa jeshi la Kenya waliokuwemo ndani ya helikopta ya…

Prof. Gurnah kubariki Tuzo ya Mwalimu Nyerere

Prof. Gurnah kubariki Tuzo ya Mwalimu Nyerere

DAR ES SALAAM: Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya mwaka 2021 katika fasihi, Prof. Abdulrazak Gurnah, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu. Hafla hiyo itafanyika kesho katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam. Akizungumza leo Aprili 12, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya…

Judith Suminwa Tuluka ateuliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kongo DR

Judith Suminwa Tuluka ateuliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kongo DR

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua waziri wa mipango Judith Suminwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Suminwa ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo wa uwaziri mkuu nchini Kongo DR. Uteuzi wa Suminwa unakamilisha wiki kadhaa  zilizogubikwa na hali ya sutafahamu kuhusu wadhifa huo. Katika hotuba aliyotoa kupitia televisheni ya taifa,…

Rais Samia atangaza siku 7 za maombolezo kufuatia kifo cha Ali Hassan Mwinyi

Rais Samia atangaza siku 7 za maombolezo kufuatia kifo cha Ali Hassan Mwinyi

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kilichotokea jana. Taarifa zaidi zinasema kuwa, katika kipindi hiki cha maombolezo ya kitaifa bendera zitapepea nusu mlingoti. Nina huzuni kutangaza kifo hiki,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan, na kuongeza…

Sheikh Zakzaky: Adui amewaua Wapalestina 20,000 dhidi ya wapiganaji 4,000.

Sheikh Zakzaky: Adui amewaua Wapalestina 20,000 dhidi ya wapiganaji 4,000.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ameeleza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni chimbuko la wahyi kwa mataifa ya Kiislamu dhidi ya madhalimu wenye kiburi, na kuhusu vita vya Ghaza amesema kua: wakati idadi ya wapiganaji wa Hamas ni 4,000 tu, adui ameua zaidi ya Wapalestina 20,000 hadi sasa, na Wengi wao katika…