CNN: Utumiaji wa Iran wa zana za mafuta ishara mbaya kwa Marekani
CNN iliandika katika ripoti yake kwamba Iran ina hiyari ya kufanya uamuzi unaoweza kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta kwa viwango vya juu zaidi ikilinganishwa na rekodi za awali, na ongezeko hili litakuwa na madhara makubwa kwa Marekani na uchumi wa dunia nzima. Kufuatia wasiwasi wa kusita kwa usambazaji wa mafuta ya Iran, bei ya…
Waislamu wapendekeza mgombea wa tatu katika uchaguzi wa rais Marekani
Licha ya mgombea urais wa chama cha Democratic, Kamala Harris, kuwa na nafasi nzuri zaidi na kumtimulia kivumbi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, katika kura za maoni za hivi karibuni, kura za Waislamu wa Marekani sasa zimeweka kipaumbele kwa mgombea wa Chama cha Kijani, Jill Stein, ambaye anaunga mkono waziwazi kadhia ya…
Amnesty International yaalaani ukandamizaji wa uhuru kabla ya uchaguzi wa rais Tunisia
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa serikali ya Tunisia kukomesha ukandamizaji unaoongezeka dhidi ya uhuru wa kimsingi kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 6 Oktoba, 2024. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kwamba, kuongezeka kwa kesi za kuwekwa kizuizini kiholela kwa wanasiasa wa upinzani, kutengwa kwa wagombea na ukiukaji…
Ufisadi Serikalini unawafanya vijana wengi wa Kiafrika wahajiri na kukimbilia Ughaibuni
Karibu asilimia 60 ya vijana wa Kiafrika wanataka kuzihama nchi zao kwa sababu serikali zao hazishikiki kwa ufisadi. Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa kwa vijana katika mataifa 16 ya Afrika. Matokeo ya uchunguzi huo yaliyotolewa siku ya Jumanne yanaeleza kuwa, vijana katika nchi hizo 16 za Afrika wamesema, ufisadi ni kikwazo…
Maandamano yasiyo na mfano nchini Israeli hii leo katika maeneo tofauti
Maandamano ya kupinga serikali nchini Israel hii leo yametofautiana na maandamano ya hapo awali katika kipindi cha vita, kulingana na Ori Goldberg, mchambuzi wa kisiasa. “Watu ambao wamekuwa wakiandamana kwa ajili ya mateka hadi sasa … [walichukuliwa] kwa ujumla kuwa sawa na watu ambao walikuwa wakiandamana dhidi ya Netanyahu kwa mwaka mmoja kabla ya vita…
Kwa nini “Israeli” iliundwa?
Mwamko wa Kiislamu ni mwanzo wa mwisho wa nchi za Magharibi na kuhodhishwa kwake katika utawala wa dunia, hivyo basi, kuchunguza vipimo vya uungaji mkono wa nchi zote za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni katika mashambulizi ya kikatili na vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa Ghaza kunaweza kufichua sababu. kwa uumbaji wa…
Harris atupilia mbali uwezekano wa kuiwekea Israel vikwazo vya silaha, adai ina haki ya ‘kujilinda’
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ametupilia mbali kwa msisitizo uwezekano wa nchi hiyo kuuwekea vikwazo vya silaha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unaoendeleza vita vya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro. Harris ameeleza hayo katika mahojiano yake ya kwanza aliyofanyiwa na televisheni ya CNN tangu awe…
UN yakosoa azma ya Israel ya kujenga sinagogi katika Msikiti wa al-Aqsa
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali pendekezo lililotolewa hivi karibuni na Waziri wa Usalama wa Israel, Itamar Ben Gvir, la kutaka kujenga sinagogi ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa. Stephane Dujarric amesema katika kikao na waandishi wa habari kuwa, “kauli za aina hii hazina tija wala maana. Zinazidisha hatari ya kushadidisha hali ambayo tayari ni mbaya.” Huku…