Mpalestina Khader Adnan akata roho na kufa shahidi akiwa ndani ya gereza la Israel
Wizara inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa mateka na walioachiwa huru imetangaza kuwa Sheikh Khader Adnan, mfungwa Mpalestina amekata roho na kufa shahidi ndani ya gereza la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Adnan, mmoja wa viongozi wa harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina, alikamatwa na utawala wa Kizayuni Februari 5 na kuamua kususia kula kwa muda wa…
Onyo la Umoja wa Mataifa kuhusu kusambaratika hali ya kibinadamu nchini Sudan
Martin Griffiths, mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kabla ya kuelekea nchini Sudan kwamba hali ya kibinadamu nchini humo ni mbaya sana kiasi kwamba imefikia kwenye hatua ya kusambaratika kabisa. Amesema, utatuzi wa mgogoro wa Sudan hauwezi kupatikana kutokana na kuendelea vita hivyo. Afisa huyo wa ngazi za juu wa Umoja…
Waziri auawa kwa kupigwwa risasi na mlinzi wake nchini Uganda
Kanali Charles Okello Engola, Waziri wa nchi katika masuala ya Ajira, Leba na Mahusiano ya Viwanda ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake mapema leo Jumanne asubuhi wakati alipokuwa anaingia kwenye gari lake kuelekea kazini. Jeshi la Polisi la Uganda limethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, waziri huyo amepigwa risasi nyumbani kwake Kyanja na mlinzi…
Wasia wa Shahidi Khizr Adnan
“Esraa Al-Bahisi” ripota wa Habari ameripoti kuhusu wasia ulioandikwa na mfungwa wa Kipalestina na shahidi mwanajeshi Khizr Adnan kabla ya kuuawa shahidi. Usia ulioandikwa na shahidi Sheikh Khizr Adnan kwa mkewe, watoto wake na watu wote waliodhulumiwa wa Palestina ni kama ifuatavyo: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema “Wale walioamini hawana khofu juu…
Hali mbaya katika jela za utawala unaoukalia kwa mabavu baada ya tangazo la kuuawa shahidi Khizr Adnan
Hali katika jela za utawala ghasibu wa Kizayuni katika kukabiliana na kuuawa shahidi Sheikh Khizr Adnan, mateka wa Kipalestina katika jela za utawala huo ghasibu, inaripotiwa kutokuwa shwari, na wafungwa wa Kipalestina waliitikia pakubwa habari za kuuawa shahidi Khizr. Adnan. Ripota wa habari mjini Ramallah ameripoti kuwa jela za utawala huo ghasibu zilishuhudia mapigano makali…
Majibu ya jeshi la anga la Syria kwa shambulio la utawala wa Kizayuni
Duru rasmi za Syria ziliripoti mapema Jumamosi kwamba ulinzi wa anga wa jeshi la nchi hiyo ulizima hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Homs. Shirika rasmi la habari la Syria; SANA, ikithibitisha habari hii, imetangaza kuwa ulinzi wa anga wa jeshi la Syria umekabiliana na makombora ya Kizayuni huko Homs na kuangamiza baadhi yao….
Iran: ‘Janga’ linalowakumba Wapalestina linakaribia kumalizika
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema ukombozi wa Palestina na mwisho wa hali ya janga ambalo Wapalestina wanakabiliwa nalo unakaribia kwani utawala wa Kizayuni wa Israel unaonekana kuwa dhaifu kuliko hapo awali. Nasser Kana’ani alitoa matamshi hayo katika taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Ijumaa kabla ya kumbukumbu chungu…
Raia watatu wajarehiwa katika shambulio la Wazayuni dhidi ya Syria
Shambulio la alfajiri la utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria lilisababisha kujeruhiwa kwa raia watatu na kuchomeka kwa kituo cha mafuta pamoja na meli kadhaa za mafuta na lori moja. Kufuatia shambulio la mapema asubuhi la utawala wa Kizayuni katika viunga vya mji wa Homs, chanzo cha kijeshi cha Syria kilitoa ufafanuzi kuhusiana na hilo….