Ubahai

Mapigano yameanza tena katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum

Mapigano yameanza tena katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum

Ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kuwa mapigano yamezuka upya kati ya vikosi vya jeshi la Sudan vinavyoongozwa na Jenerali Abdel-Fattah al-Barhan na vikosi vya Radiamali ya Haraka RSF vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Daghlo maarufu kama Hamidati katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum. Chaneli ya televisheni ya Al-Jazeera imetangaza mapema leo kuwa mapigano kati ya…

Mapigano ya kutumia silaha katika kambi ya Jenin/ Wapalestina 8 wajeruhiwa

Mapigano ya kutumia silaha katika kambi ya Jenin/ Wapalestina 8 wajeruhiwa

Duru za Palestina zimeripoti kuwa, Wapalestina 8 walijeruhiwa kwa risasi za kivita katika mapigano ya silaha kati ya wapiganaji wa muqawama na wanajeshi wa Kizayuni katika kambi ya Jenin. Wanajeshi wa Israel walivamia nyumba za raia wa Palestina na wavamizi waliwekwa kwenye paa za baadhi ya nyumba. Duru za Palestina zilizonukuliwa na redio ya utawala…

Wapiganaji wa Kipalestina walipambana na askari wa Kizayuni mjini Jenin

Wapiganaji wa Kipalestina walipambana na askari wa Kizayuni mjini Jenin

Mapema leo Jumatano wapiganaji wa Kipalestina wamekabiliana vikali na utawala wa Kizayuni katika eneo la Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Vyanzo vya habari kwa kuchapisha faili za video vimebainisha kuwa kufuatia shambulio la jeshi la Kizayuni dhidi ya makazi ya Qabatiya kusini mwa mji wa Jenin, sauti ya risasi na mapigano kati…

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria: Mashambulio ya Israel bila shaka yatajibiwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria: Mashambulio ya Israel bila shaka yatajibiwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria ameeleza kuwa, ziara za pamoja za viongozi wa Damascus na nchi za Kiarabu ni kwa irada na matakwa ya pande zote, na kusisitiza kwamba, jibu la Syria kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni ni jambo lisiloepukika. Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Al-Maqdad, aliyetembelea Algiers jana,…

Hadithi kuhusu “mshtuko wa ubongo” kwa wanajeshi wa Amerika?

Hadithi kuhusu “mshtuko wa ubongo” kwa wanajeshi wa Amerika?

Kamandi Kuu ya Marekani ilitangaza kwamba wanajeshi 23 wa Kimarekani nchini Syria walipatwa na mshtuko wa ubongo kutokana na mashambulizi ya watu waliokua na silaha mnamo mwezi wa Machi mwaka jana. Amri hii ilisema katika taarifa: Kesi 11 mpya za mishtuko midogo midogo zimesajiliwa katika vikosi vya Amerika wakati wa shambulio la Machi 23 na…

Mapigano ya kuwania madaraka baina ya majenerali yaingia siku ya pili nchini Sudan

Mapigano ya kuwania madaraka baina ya majenerali yaingia siku ya pili nchini Sudan

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Radiamali ya Haraka yameingia siku ya pili, huku milipuko ikisikika tangu alfajiri ya leo, Jumapili, karibu na Mji wa Michezo, kusini mwa mji mkuu, Khartoum. Hali ya sintofahamu inaendelea kutanda kuhusu yanayojiri katika medani ya vita kutokana na taarifa zinazokinzana zinazotolewa na pande hasimu. Hadi sasa watu zaidi…

Tovuti 60 za utawala wa Kizayuni zililengwa katika shambulio la kimtandao

Tovuti 60 za utawala wa Kizayuni zililengwa katika shambulio la kimtandao

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti Jumamosi usiku kwamba tovuti 60 za utawala huu ziliharibiwa na mashambulizi ya mtandaoni katika muda wa siku 2 zilizopita. Kanali ya 12 ya utawala wa Kizayuni imeripoti kuwa, shambulio hilo la mtandao ni shambulio kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni ambalo limelenga mkusanyiko mkubwa wa tovuti…

Mjumbe wa Baraza Kuu la Yemen: Tumejiweka tayari kwa chaguo lolote lile itakaloamua Saudia

Mjumbe wa Baraza Kuu la Yemen: Tumejiweka tayari kwa chaguo lolote lile itakaloamua Saudia

Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema, “tumejiweka tayari kwa machaguo yote; ikiwa muungano wa Saudia utataka suluhu, sisi ni watu wa suluhu na ikiwa wanataka vita pia, sisi tumepata uzoefu wake kwa miaka minane”. Siku mbili zilizopita, jumbe za Saudi Arabia na Oman ziliwasili mji mkuu wa Yemen, Sana’a kwa lengo la kukutana…