Ubahai

Saudi Arabia imelaani kauli za Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni kuhusu Palestina

Saudi Arabia imelaani kauli za Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni kuhusu Palestina

Katika taarifa yake siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imelaani matamshi ya matusi na ya kibaguzi yaliyotolewa na Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa la Palestina. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Saudi Arabia imesema kuwa kuita matamshi yaliyo kinyume na ukweli kueneza matamshi ya chuki na…

Safari ya Rais Assad UAE: Syria kurejea tena katika Jumuiya ya Arab League

Safari ya Rais Assad UAE: Syria kurejea tena katika Jumuiya ya Arab League

Rais Bashar al-Assad wa Syria jana aliwasili katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu na kulakiwa rasmi na Rais Mohammed bin Zayed al-Nahyan ikiwa ni ishara ya wazi ya kuhuishwa uhusiano wa Syria na mataifa ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi baada ya zaiidi ya muongo mmoja. Hii ni ziara ya pili ya Rais…

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni atishia kujiuzulu

Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni atishia kujiuzulu

Waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni alitoa onyo kwa baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni ya kwamba atajiuzulu iwapo mageuzi ya mahakama yatafanyika. Yoaf Gallant, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni alitishia kujiuzulu kwa baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu. Kanali ya 13 ya utawala wa Kizayuni…

Uwezekano wa kutumwa kwa wanajeshi 300,000 wa NATO barani Ulaya ili kukabiliana na Urusi

Uwezekano wa kutumwa kwa wanajeshi 300,000 wa NATO barani Ulaya ili kukabiliana na Urusi

Duru za habari zilidai kuwa NATO inapanga kuimarisha mipaka yake ya mashariki na kutuma kiasi cha wanajeshi 300,000 katika nchi zinazopakana na Urusi. Vyanzo vya habari vilidai Jumapili kuwa NATO inapanga kusimamisha Urusi ikiwa itaamua kupanua vita zaidi ya Ukraine. Kwa sababu hiyo, muungano unaoongozwa na Marekani unapanga kuimarisha mipaka yake ya mashariki na kutuma…

Atakayemkabidhisha askari wa Ukraine aliyeivunjia heshima Qur’ani kuzawadiwa $168,000

Atakayemkabidhisha askari wa Ukraine aliyeivunjia heshima Qur’ani kuzawadiwa $168,000

Rais Madan Kadyrov, wa eneo la Russia linalojiendeshea mambo yake la Chechnya ametenga zawadi ya ruble milioni 10 za Kirusi ambazo ni sawa na dola 168,000 za Kimarekani kwa atakayefanikisha kukamatwa akiwa hai, askari wa jeshi la Ukraine aliyeivunjia heshima Qur’ani tukufu kwa kuichoma moto nakala ya kitabu hicho kitakatifu. Tovuti ya kituo cha habari…

Ujumbe muhimu zaidi wa mazoezi ya pamoja kati ya Iran, Urusi na China

Ujumbe muhimu zaidi wa mazoezi ya pamoja kati ya Iran, Urusi na China

Amir Admiral Shahram Irani, kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza ulazima wa kudhaminiwa usalama katika eneo kwa kusisitiza kuwa, nchi za eneo hili ni katika vyanzo vikubwa zaidi vya mafuta duniani. Amiri wa Iran amemwambia ripota wa kituo cha habari cha Al-Alam kwamba nchi zote za eneo hilo zina…

Kampuni ya Ufaransa yaacha tani milioni 20 za sumu nchini Niger, hofu yatanda

Kampuni ya Ufaransa yaacha tani milioni 20 za sumu nchini Niger, hofu yatanda

Kampuni moja ya Ufaransa inajitahidi kuondoa takriban tani milioni 20 za taka za sumu zenye mionzi ambazo zilisalia kufuatia kufungwa kwa shughuli zake katika migodi mikubwa ya madini ya uranium katika eneo la Arlit kaskazini mwa Niger. Kampuni kubwa ya nyuklia ya Ufaransa, Areva, ambayo ilibadilisha jina lake kuwa Orano, ilifanya kazi katika eneo la…

Mufti wa Oman: Mapatano ya Iran na Saudia yameutia hofu na kiwewe utawala wa Kizayuni wa Israel

Mufti wa Oman: Mapatano ya Iran na Saudia yameutia hofu na kiwewe utawala wa Kizayuni wa Israel

Mufti wa Oman Sheikh Ahmad bin Hamad Al-Khalili amesisitiza haja ya kudumishwa amani na utangamano katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kubainisha kwamba, makubaliano na mapatano yaliyofikiwa kati ya Iran na Saudi Arabia yameutia hofu na kiwewe utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Kufuatia mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya…