Hofu ya Wazayuni juu ya uwezekano wa kurudi kwa uhusiano wa kawaida kati ya Iran na Misri
Baada ya makubaliano hayo kati ya Iran na Saudi Arabia, hivi sasa vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vinazungumzia wasiwasi na hofu ya mamlaka ya Tel Aviv kuhusu kuhalalisha uhusiano kati ya Tehran na Cairo katika siku za usoni. Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina “Sama”, tovuti ya habari ya “Makor Rashon”…
Vikosi maalum vya Kizayuni: Hatutahudumu jeshini kuanzia Jumapili
Vikosi mia moja vya akiba vya operesheni maalum ya utawala wa Kizayuni vilitangaza Alhamisi usiku kwamba havitahudumu katika jeshi kuanzia Jumapili katika harakati ya kupinga mageuzi ya mahakama. Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti kuwa mamia ya vikosi maalum vya akiba vya idara ya ujasusi ya kijeshi, Mossad na Shabak vilitangaza kuwa havitaendeleza…
Vikosi vya muqawama vya Palestina vyafanya operesheni 22 dhidi ya Wazayuni
Duru za habari zimeripoti hivi karibuni kwamba, wanajeshi wa muqawama wa Palestina walifanya oparesheni 22 dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika muda wa saa 24 zilizopita. Kituo cha Takwimu na Habari cha Palestina kinachojulikana kwa jina la “Mu’ti” kilitangaza kuwa, vikosi vya muqawama vya Palestina vilifanya operesheni 22 dhidi ya…
Kejeli za Lapid kwa Netanyahu: baraza la mawaziri linaendeshwa na mtu mwengine
Yair Lapid, Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa sasa wa upinzani katika baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu, alimwambia Waziri Mkuu wa Israel kwa maneno ya kejeli: “Ushahidi na nyaraka tulizopokea usiku wa leo ni kwamba Bibi hadhibiti baraza lake la mawaziri.” Akijibu kukataa kwa Netanyahu ombi la Rais wa Israel Isaac Herzog kuhusu…
Russia yaitaka Marekani isitishe safari za ndege ‘za uhasama’ baada ya tukio la droni
Balozi wa Russia nchini Marekani anasema “vitendo visivyokubalika” vya jeshi la Marekani karibu na ardhi ya Russia ni “sababu ya wasiwasi,” huku akiitaka Washington kusimamisha safari “za ndege za uhasama” karibu na mipaka ya nchi hiyo. Anatoly Antonov alisema hayo katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Telegram siku ya Jumatano, siku moja baada ya Moscow…
Safari ya Netanyahu nchini Ujerumani huku maandamano ya Wazayuni yakiendelea
Serikali ya Ujerumani ilitangaza kuwa kansela wa nchi hiyo atakuwa mwenyeji wa waziri mkuu wa Israel katika mkutano wa “chakula cha mchana” mjini Berlin Alhamisi hii. Afisa wa Ujerumani alitangaza mpango wa Waziri Mkuu Olaf Schultz kwa ajili ya mkutano wa pande mbili na Benjamin Netanyahu huko mjini Berlin. Vyanzo vya habari kutoka Berlin, mji…
Idadi kubwa ya Wapalestina yatiwa nguvuni na jeshi la Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Vikosi vya Kizayuni vinavyoikalia kwa mabavu vilianza oparesheni ya kuvamia, kusaka na kukamata Wapalestina katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu kuanzia alfajiri ya leo (Jumatatu). Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni waliwatia mbaroni ndugu wanne waliojulikana kwa majina Muhammad, Bara, Abdul Rahman na Momin Qarawi kutoka kambi ya…
Afisa wa jeshi la Iraq: Zaidi ya wanachama 400 wa ISIS bado wako Iraq
Afisa wa jeshi la Iraq amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) bado lina wapiganaji 400 hadi 500 katika nchi hiyo. Qais Al-Mohammadawi, Naibu wa Kamandi ya Operesheni ya Pamoja, ambayo inasimamia ushirikiano wa vikosi vya usalama vya Iraqi na muungano wa kimataifa, ametangaza kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS nchini Iraq…