Russia imelaani vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni nchini Syria
Huku ikilaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Syria, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imetahadharisha kuhusu kushadidi kwa mizozo ya kijeshi kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo. Siku ya Ijumaa, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia ililaani mashambulizi ya kuendelea na haramu ya utawala wa Kizayuni katika nchi ya Syria na kuonya…
Madai ya mara kwa mara ya Ikulu ya Marekani: Tuko tayari kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya 2015 na Iran
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema Jumanne jioni katika madai ya mara kwa mara kwamba Washington iko tayari kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya 2015 na Iran. Msemaji wa Ikulu ya White House, Karin Jane Pir alisema Jumanne jioni kwamba ikiwa Iran iko tayari kuzingatia makubaliano ya nyuklia ya 2015, tuko tayari kufanya vivyo hivyo….
Mkusanyiko wa kulalamikia kufukuzwa nchini Ufaransa Imam wa Swala ya Jamaa
Mwenendo wa chuki dhidi ya Uislamu na vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu katika mataifa ya Ulaya hususan Ufaransa ungali unaendelea. Katika fremu hiyo, Baraza la Utawala la Ufaransa, limeidhinisha hukumu ya kufukuzwa nchini humo Hassan Iquioussen Imam wa Swala ya Jamaa mwenye asili ya Morocco kwa tuhuma za kueneza chuki dhidi ya Mayahudi. Pamoja na…
Timu zote 5 za Afrika mara hii zinaongozwa na makocha wazawa katika kombe la dunia Qatar
Kombe la Dunia la Qatar 2022 litakuwa la kihistoria kwa mchezo wa soka barani Afrika, kwa sababu nchi zote tano za bara hilo zinazoshiriki katika michuano ya kuwania kombe hilo ambazo ni Morocco, Senegal, Cameroon, Tunisia na Ghana zitaongozwa na makocha Waafrika. Kwa mujibu ripoti ya toleo la leo la gazeti la Kayhan, kocha Mbosnia…
Russia yasisitiza kuhamishwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka New York
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesisitiza kuwa Moscow inazingatia kikamilifu pendekezo la kuhamisha makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutoka Marekani hadi sehemu nyingine. Alexey Drobinin, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema: “Katika miaka ya mwanzo mwa kuasisiwa Umoja wa Mataifa, wakati pande zote zilikubali kwamba makao…
Kugonga mwamba juhudi za Israel za kuanzisha uhusiano wa kawaida na Pakistan
Viongozi kadhaa wa kidini, kisiasa, wanafikra na wasomi wa Kipakistan wamesema katika kongamano la kifikra kuhusu Palestina kwamba, juhudi za hivi karibuni za Marekani na vibaraka wake za kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Pakistan na Israel zimegonga mwamba. Mkutano wa Kamati ya Kuunga Mkono Jumuiya ya Palestina nchini Pazkistan ulifanyika Ijumaa iliyopita ya Septemba…
Wanajeshi wa Israel wamuua kijana Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi
Vikosi vya kijeshi vya utawala ghasibu wa Israel vimempiga risasi na kumuua shahidi kijana mwingine wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo siku ya Jumatatu. Mpalestina huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 alipigwa risasi na kuuawa na jeshi la Israel wakati wa uvamizi mapema Jumatatu huko Qabatiya, kusini mwa…
Kununuliwa ardhi kwa ajili ya Wazayuni; juhudi za kuyahudishwa Manama
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya al-Wifah nchini Bahrain amesema kuna mpango wa siri unaotekelezwa kwa lengo la kuanzisha mtaa wa Mayahudi katika sehemu kongwe ya Manama, mji mkuu wa Bahrain. Tangu mwaka 2020, Bahrain imeanzisha uhusiano wa wazi wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel unaokalia kwa mabavu Quds Tukufu, na uhusiano huo umekuwa…