HAMAS: Vita dhidi ya Israel vitaendelea mpaka mateka wote wa Kipalestina watakapoachiliwa huru
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa, vita dhidi ya utawala haramu wa Israel vitaendelea mpaka pale mateka wote wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala huo ghasibu watakapoachiliwa huru. Hayo yameelezwa na Zaher Jabarin, afisa wa Hamas anayeshughulikia faili la mashahidi na mateka wa Palestina na kueleza kwamba, harakati hiyo haitapata utulivu na…
Wapiganaji wa Tigray wadai kuwateka nyara mamia ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia
Wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) ya kaskazini mwa Ethiopia wametangaza kuwa, wanawashikilia mamia ya wanajeshi wa serikali iliowateka nyara hivi karibuni. Taarifa hiyo ambayo haikutoa maelezo zaidi imedai kwamba, hivi sasa mamia ya wanajeshi wa serikali wanashikiliwa na wapiganaji hao. Kadhalika wanamgambo hao wamedai kuwa, wanajeshi wa Ethiopia wamekuwa wakiwatumia watoto…
Kupamba moto vita vya nishati barani Ulaya
Suala la kudhaminiwa mahitaji ya gesi kwa nchi za Ulaya sasa limekuwa tatizo sugu kwa nchi hizo. Nchi za Ulaya, ambazo ziliamua kuiwekea Russia vikwazo vya kila aina ili kuishinikiza katika vita vya Ukraine, sasa zinaituhumu Moscow kwamba inaitumia gesi kama silaha ya vita. Kabla ya kuanza vita vya Russia na Ukraine, Moscow ilikuwa moja…
Iran: Matukio ya karibuni ya Ukraine ni matunda ya uingiliaji wa Marekani
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa, Marekani na nchi za Magharibi zinataka kutekeleza siasa zao za kibeberu katika maeneo yote hassasi na ya kiistratijia duniani na kwamba matukio ya Ukraine ni matunda ya mtazamo huo wa kiistikbari wa Magharibi. Shirika la habari la FARS limemnukuu Brigedia Jenerali Mohammad-Reza Gharaei Ashtiani akisema hayo jana wakati alipoonana na…
Yemen: Tuna uwezo wa kupiga popote katika maji yanayoizunguka nchi yetu
Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, nchi hiyo ina uwezo wa kupiga na kushambulia katika sehemu yoyote ya maeneo ya majini yaliyoko karibu na Yemen. Televisheni ya Almasirah imetangaza habari hiyo leo Ijumaa na kumnukuu Mahdi al Mashat akisema hayo wakati wa gwaride kubwa la kijeshi lililofanyika kwenye mkoa wa al Hudaidah…
Umoja wa Mataifa: China imekiuka haki za binadamu za Waislamu wa Xinjiang
Umoja wa Mataifa umetoa ripoti inayoeleza kufanyika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya Waislamu wa jamii ya Uighur katika jimbo la Xinjiang nchini China. Ripoti hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet imeeleza kuwa, madai ya mateso ni kweli na kuna uwezekano kwamba…
IRGC ya Iran yaeleza ilivyotwaa na kuachia huru droni ya Marekani
Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa maelezo ya kina kuhusu namna lilivyoteka na kisha kuachia huru ndege isiyo na rubani ya baharini ya Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi. IRGC imefafanua kuwa, imetoa maelezo hayo ili kujibu madai ya kuchekesha ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani katika eneo la…
Meja Jenerali Salami: Majeshi ya Iran yako tayari kujibu vitisho vya maadui
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Iran ni ya ajabu, yenye kuonyesha nguvu na yenye uwezo wa kumzuia adui huku akisisitiza kuwa: “Vikosi vya kijeshi vya Iran viko tayari kujibu vitisho vya adui.” Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi…