Mapitio ya barua ya kihistoria ya Imam Khomeini (RA) kwa Gorbachev
Mikhail Gorbachev, kiongozi wa mwisho wa Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Sovieti (Union of Soviet Socialist Republics, USSR) alifariki dunia Jumanne usiku katika hospitali moja mjini Moscow, Russia akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa mnasaba wa kifo cha Gorbachev, tunalifanyia mapitio moja ya matukio muhimu zaidi yaliyojiri katika…
Rais wa Lebanon: Misimamo ya Imamu Musa Sadr inatoa ilhamu kwetu sote
Rais Michel Aoun wa Lebanon amesema, misimamo ya Imamu Musa Sadr ni chemchemi ya ilhamu kwa Walebanon wote ili wafanye juhudi kwa ajili ya ukombozi wa nchi na watu wake. Rais wa Lebanon ameyasema hayo kwa mnasaba wa kukumbuka siku aliyotekwa nyara Imamu Musa Sadr alipokuwa safarini nchini Libya. Kwa mujibu wa tovuti ya habari…
Israel yaua shahidi Wapalestina 2; yashambulia Syria kwa makombora
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendeleza jinai na chokochoko zake dhidi ya mataifa mawili ya Waislamu katika eneo hili la Asia Magharibi. Wanajeshi makatili wa utawala huo pandikizi wamewaua shahidi mabarobaro wawili wa kiume wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kituo cha Habari cha Palestina kimeripoti kuwa, vijana hao wa Kipalestina Yazan Afana…
Kanada na Uingereza zilishirikiana kusafirisha wasichana kujiunga na magaidi wa Daesh
Idara ya ujasusi ya Kanada ilihusika katika kutuma wasichana kwenda kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na serikali ya Uingereza ilijua nafasi ya Kanada katika kashfaa hiyo lakini ikajizuia kuifichua. Hayo yamefichuliwa na mwandishi ambaye anaeleza kuhusu kisa cha Shamima Begum, raia wa zamani wa Uingereza ambaye alijiunga na ISIS mwaka 2015 akiwa na…
Shambulio la kombora la Israel kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aleppo
Vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aleppo ulioko kaskazini magharibi mwa Syria ulishambuliwa kwa makombora kadhaa. Vyanzo hivyo viliripoti kua sauti ya milipuko kadhaa ilisikika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aleppo Jumatano jioni. Likithibitisha habari hii, shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa milio…
Russia: Mashambulizi dhidi ya Syria yamefichua undumakuwili wa Magharibi
Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali mashambulio haramu ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa, hujuma hizo zimefichua sura halisi ya Wamagharibi likija suala la haki za binadamu. Vasily Nebenzia amesema hayo katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, “Israel…
Waziri Mkuu wa Japan aahidi kufuatilia kiti cha Afrika katika Baraza la Usalama
Waziri Mkuu wa Japan amesema kuwa, nchi yake ina mpango wa kustafidi na nafasi na ushawishi wake katika Baraza la Usalama ili kuhakikisha kuwa, bara la Afrika linapatiwa kiti cha kudumu katika taasisi hiyo muhimu duniani. Fumio Kishida, Waziri Mkuu wa Japan amesema hayo katika hotuba yake kwenye “Mkutano wa Kimataiifa wa Tokyo Kwa Ajili ya Ustawi…
Amir-Abdollahian: Iran inafuatilia kuhakikisha kunafikiwa makubaliano ya kudumu katika mazungumzo ya Vienna
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mazungumzo ya Vienna ya kuondolewa vikwazo taifa hili na kusema kuwa, Tehran inafuatilia kwa nguvu zote kuhakikisha kunafikiwa makubaliano ya kudumu. Hussein Amir-Abdollahian, amesema hayo katiika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Moscow akiwa pamoja na mwenyeji wake, Sergey Lavrov, Waziri wa…