Sheikh Issa Qassim: Kujengwa kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi Manama ni jinai
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amekosoa viikali uamuzi wa utawala wa Aal Khalifa wa kuanzisha kitongoji cha walowezi wa Kiyahudi katika mji mkuu Manama na kueleza kwamba, hatua hiyo ni jinai na dhulma ya wazi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu. Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa Mapinduzi ya Wananchi wa…
Russia: Marekani irejeshe fedha za Afghanistan zilizoibwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani izirejeshe fedha zilizoibiwa Afghanistan. Vasily Nebenzya ametoa mwito huo alipohutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Russia TASS, mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kujadili suala la Afghanistan uligeuka uwanja wa utoaji tuhuma…
Wamarekani: Ndani ya miaka 10 ijayo vita vya wenyewe kwa wenyewe vitatokea nchini
Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni yanaonyesha kuwa zaidi ya 40% ya Wamarekani wanaamini kwamba ndani ya miaka 10 ijayo, vita vya wenyewe kwa wenyewe vitatokea nchini humo. Kugunduliwa hati zaidi ya 300 zenye muhuri wa siri kwenye nyumba ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kumeshadidisha mvutano kati ya serikali ya Wademocrat na Trump…
Sisitizo la kuendelezwa “medani za pamoja za mapambano” na kuangaliwa Israel kama adui wa pamoja wa Wapalestina wote
Huku utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ukiwa umeanzisha vita vikali vya kisaikolojia katika siku za hivi karibuni kuulenga uhusiano wa Hamas na Jihadul-Islami, viongozi wa harakati hizo mbili za muqawama za Palestina wamesisitiza katika mazungumzo yao kwamba wameungana na wako kitu kimopja katika mapambano yao dhidi ya utawala huo ghasibu. Hivi karibuni, utawala wa…
Muqtada Sadr na machafuko ya Iraq
Jumapili ya jana tarehe 29 Agosti Iraq Jumapili ilishuhudia sokomoko na matukio ambayo kimsingi yalitabiriwa kutokea. Wimbi la machafuko hayo lilienea huku chanzo na chimbuko lake likiwa ni mwenendo wa kisiasa wa Muqtada Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Sadr ya Iraq. Jumapili ya jana Ayatullah Hairi Marjaa Taqlidi wa Kishia ambaye anatambuliwa na wengi kama muungaji mkono wa…
Putin apongeza ushirikiano wa nchi za Kiislamu katika kutatua masuala ya kimataifa
Katika ujumbe wake Vladimir Putin, hii leo amesifu hatua ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu na Russia katika kutatua masuala ya kimataifa. Shirika la habari la Tass leo hii limenukuu ujumbe wa Rais wa Russia kwa washiriki na wageni wa Kongamano la Vijana Ulimwenguni huko Kazan na kusema: Nchi za Kiislamu zimekuwa washirika wa jadi…
Ikulu ya Marekani: Hali nchini Iraq inatia wasiwasi
Ikikanusha taarifa za kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, Ikulu ya White House iliitaja hali ya Iraq kuwa yenye kutia wasiwasi na kutoa wito wa kudumisha amani na kuwepo kwa mazungumzo. Siku ya Jumatatu, Ikulu ya Marekani ilidai kuwa taarifa za kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Iraq si za kweli.Taarifa kuhusu kuhamishwa kwa…
Wanachama kadhaa wa Umoja wa Ulaya wapinga vikwazo dhidi ya Russia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland amesema kuwa, kuna wanachama kadhaa wa Umoja wa Ulaya wanapinga vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia. Shirika la habari la Sputnik limemnukuu Péter Szijjártó akisema hayo na kuongeza kuwa, Poland haina hata hamu ya kuzungumzia vikwazo zaidi vya Magharibi dhidi ya Russia hususan linapokuja suala la mafuta…